Simba ya safari hii haitanii, yaichapa Azam 2-0
Simba ya safari hii haina utani hata kidogo kwani usiku huu imeichapa Azam FC mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu bara kwenye uwanja wa New Amaan Zanzibar.
Lionel Ateba dakika ya 15 aliifungia Simba SC bao la uongozi kabla ya Fabrice Luamba Ngoma dakika ya 47 kufunga la pili.
Hata hivyo goli la pili lililofungwa na Ngoma, linadaiwa ni off side lakini waamuzi wa mchezo huo wakiongozwa na Elie Sasii alikubaliana na goli hilo.
Kwa ushindi huo Simba imefikisha pointi 9 ikiwa imecheza mechi 3 na inazidi kuiacha nyuma Yanga ambayo jana ilipata ushindi kiduchu dhidi ya KenGold
.