Yanga yashinda kiduchu
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara Yanga SC jioni ya leo imeibuka na ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi ya KenGold katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara.
Kwa ushindi huo Yanga imefikisha pointi 6 na mechi mbili huku ikiendelea kusaka ushindi kwenye mechi ijayo dhidi ya KMC.
Bao pekee la Yanga limefungwa na Ibrahim Baka dakika ya 13 kipindi cha kwanza, Krngold ambao kwenye mechi zake imepoteza, lakini leo imejidhatiti na kidogo wasifungwe mchezo huo kwani walilinda mno lango lao.
Mashabiki wa Yanga hawakuamini timu yao kubanwa na kuambulia ushindi kiduchu huku wakishindwa kuishusha Simba iliyombele yao