Ni marufuku kumjadili mwamuzi hata kama akiboronga
Bodi ya Ligi (TPLB) kupitia kanuni zinazosimamia ligi hiyo zinazokataza makocha, wachezaji na viongozi kuwajadili waamuzi. Kanuni ya 40 kifungu cha (2) cha Udhibiti wa Kimashindano kinaainisha kuwa:
.
“Ni marufuku kwa kocha/kiongozi wa timu/klabu, mchezaji au mdau mwingine yeyote wa mpira wa miguu kushutumu au kutoa matamshi/maandiko/picha/video kwa lengo la kumkejeli au kumshutumu au kumkashifu au kumdhalilisha mwamuzi yeyote wa mchezo/kiongozi wa TFF/FA (M)/TPLB kwenye vyombo vya habari na mahali pengine popote.
.
“Kiongozi au mdau atakayekiuka atafungiwa idadi ya michezo isiyopungua mitatu au kutojihusisha na mpira wa miguu kwa kipindi kati ya miezi mitatu mpaka kumi na miwili na au faini kati ya Sh500,000 hadi 5,000,000.