Diddy atangaza kuuza mjengo wake wa kifahari
Ni rasmi sasa rapa, producer na mfanyabishara Sean Combs 'Diddy' anauza mjengo wake uliopo Beverly Hills, California Dola Milioni 61 sawa na Tsh Bilioni 166 na ushee.
Mjengo huo aliununua mwaka 2014 dola milioni 39 Tsh Bilioni 106 una vyumba 10, ukubwa wa futi za mraba 17000, ekari 1.3, sebule kubwa, chumba cha chakula, barabara, ukumbi wa michezo, ghorofa 2 za wageni na studio ya kurekodi.
Unaambiwa mauzo ya mjengo huo inafanya kuingia orodha ya pili kwa nyumba zilizouzwa kwa bei kubwa zaidi eneo hilo la Beverly Hills.