Kesi ya Masoud Kipanya na Mwijaku yapigwa kalenda
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar imepanga kusikiliza Mapingamizi manne ya kisheria yaliyowasilishwa na Burton Mwemba (Mwijaku) dhidi ya mashtaka ya kashfa yanayomkabili kutoka kwa Masoud Kipanya, Oktoba 17, 2024 mbele ya Jaji David Ngunyale
-
Amri ya kuanza kusikiliza mapingamizi hayo kabla ya kesi ya msingi imetolewa na Jaji Ngunyale baada ya kupokea hati ya utetezi ya Mawakili wa Mwijaku, ambapo Wakili wa Kipanya alikubaliana na amri hiyo
-
Katika pingamizi hilo, Mawakili wa Mwijaku wanaiomba Mahakama ifute kesi ya msingi kwa gharama, wakidai kuna kasoro za Kisheria kama uwezo wa Mahakama kusikiliza kesi hiyo, makosa katika uthibitishaji wa maelezo, na kukosekana kwa vielelezo sahihi
-
Katika kesi ya msingi, Kipanya anamdai Mwijaku fidia ya Tsh. Bilioni 5.5 kwa kumkashfu kupitia Facebook pamoja na Mitandao mingine ya Kijamii, akihusishwa na biashara haramu na madai ya kuhongwa ili kuwachafua Viongozi wa Serikali, akiwemo Rais