Diarra achomoza Afrika

Kipa wa Yanga, Djigui Diarra, ameingia anga za makipa bora Afrika akila sahani moja na Sipho Chaine wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini kwa kucheza mechi nne za hatua ya awali katika Ligi ya mabingwa Afrika bila kuruhusu bao lolote.

Makipa hao wawili wametumia dakika 360 za mechi nne za raundi ya kwanza na ya pili bila kuruhusu bao, wakiwafunika hadi Ronwen Williams wa Mamelodi Sundowns na Mohamed El Shenawy wa Al Ahly, ambao wametumika katika dakika 180 kupitia mechi mbili kila mmoja bila kuruhsu bao lolote hadi sasa.

Diarra amekuwa nguzo muhimu kwa Yanga, akisaidia timu kufika hatua ya makundi bila kuruhusu goli, jambo linalomweka katika kundi la makipa hao.

Diarra ametumia dakika hizo katika mechi mbili za raundi ya kwanza dhidi ya Vital’O Burundi na Yanga ilishinda jumla ya mabao 10-0 ikianza kwa kushinda 4-0 na ziliporudiana ilishinda tena 6-0, kisha ikacheza mechi za raundi ya pili dhidi ya CBE SA ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 7-0.

Diarra aliendeleza umwamba kwa kuisaidia Yanga kushinda 1-0 ugenini jijini Addis Ababa, Ethiopia kisha wikiendi iliyopita ikicheza Uwanja wa Amaan Zanzibar, Yanga ilishinda tena 6-0 na kufanya kipa huyo na Yanga kwa jumla kucheza mechi nne na kufunga jumla ya mabao 17-0.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA