Nay wa Mitego alikoroga tena, aitwa BASATA
Msanii Emmanuel Elibariki, maarufu 'Nay Wa Mitego' anatuhumiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kutoa wimbo wake uitwao NITASEMA bila kibali, kinyume na taratibu za Baraza hilo
Pia, Nay Wa Mitego anadaiwa kutoa Wimbo huo wenye maudhui yanayohamasisha uchochezi dhidi ya Serikali, kuipotosha jamii kuhusu uwezo wa Rais kutekeleza majukumu yake na kukashifu mataifa mengine kama Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jambo ambalo linaweza kuleta mgogoro wa kidiplomasia kati ya Tanzania na mataifa hayo
Aidha, Hati ya Makosa imesema Wimbo wa 'NITASEMA' ulisambazwa kwa walaji kabla ya kupewa kibali cha kuthibitisha kuwa maudhui yake yamezingatia maadili yanayotakiwa