Poul Pogba anatia huruma
Nyota wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa, Poul Pogba ametoa maneno ya kushangaza ambayo aliwahi kuambiwa na baba yake zamani.
"Nilipopata mshahara wangu wa kwanza mkubwa kutoka Manchester United nilikuwa na furaha sana na baba akaniambia " mwanangu usichezee pesa maana haya yakiisha watu wote wataondoka na kukuacha mwenyewe".
Sikuelewa maneno hayo mpaka nilipopata matatizo ndipo niligundua marafiki waliyonizunguka muda wote hawaji tena kuniona.
Watu pekee niliobaki nao ni familia yangu tu.
Hayo ndio maisha. " , Alisema Pogba