Mashujaa FC yaibana mbavu Azam FC
Timu ya Mashujaa FC jioni ya leo imeilazimisha Azam FC kwenda nayo sare isiyo na mabao 0-0 katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma mchezo wa Ligi Kuu bara.
Hali sio nzuri kwa Azam ambao msimu uliopita ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya pili na kushiriki michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika.
Kwasasa Azam FC imefikisha pointi 9 ikiwa imecheza mechi 6 lakini kwa jinsi ilivyo sidhani inaweza kuwa kama msimu uliopita