Mexime ataka marefa nao wafukuzwe wakiboronga
Kocha wa Dodoma Jiji FC ya jijini Dodoma, Mecky Mexime amewashauri TFF kuwafukuza marefa wanaoboronga kama wanavyofutwa kazi wao makocha.
“Mpira hapa umechezwa wewe mwenyewe umeona vuta nikuvute, lakini vitu kama vile vinashusha thamani yetu, mbona sisi tukifanya vibaya tunafukuzwa kwenye timu, sasa wenye mamlaka kama watu wanafanya vibaya kwa nini wasiwafukuze inashindikana kitu gani ee.”
"Kama hivi ndo maana makocha wazawa tunadharaulika na hawa wageni wanakuja kuchukua hela na Kuondoka"
Mecky Maxime Kocha wa Dodoma jiji baada ya mchezo v Simba SC kuhusu waamuzi.