TRA yamzulia utata semaji la CAF
Meneja wa habari wa klabu ya Simba SC, Ahmed Ally ameomba radhi baada ya kutoa kauli iliyoleta tafrani baada ya kuitaja vibaya Mamlaka ya mapato nchini, TRA.
Kwenye mahojiano yangu leo nikitoka Dodoma kurudi Dsm, nilinukuliwa nikisema Misimu iliyopita hatukufanya vizuri kwa sababu baadhi ya Wachezaji walikuwa wameridhika na Mafanikio, hawapambani yaaani wanacheza kama Wafanyakazi wa TRA
Mfano wa TRA umeeleweka vibaya kiasi cha kuzua taharuki na kwa mantiki hiyo sina budi kuomba radhi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania na wote waliokwazika na sentensi hiyo, amesema Ahmed Ally.