Chid Benzi aamua kutembea kwa miguu kisa nauli
Msanii wa Hip Hop, Chid Benz amesema ameamua kutembea kwa miguu kutokana na madereva wengi wa bodaboda kuogopa kumbeba wakidhani hatawalipa nauli zao.
Chid maisha yake yamebadilika na mwenyewe amesema anapenda anavyoishi sasa na hata akiwa na hela hatayabadilisha.
"Maisha ninayoishi sasa hivi ni mazuri sana,watu wananipita tu hawanishangai, yaani siishi kwa uoga sababu ya watu watanionaje au waandishi wa habari wataniona.
"Haya ndiyo maisha ninayoishi na hata nikija kupata pesa niteendelea kuishi hivi, ila kuna hawa waendesha bodaboda huwa wanazingua sana.
Yaani nikiwasimamisha kutaka usafiri baadhi yao wanakataa kunipandisha wanadhani sitawalipa pesa," amesema na kuongeza ana uwezo wa kutembea kwa miguu kutoka Sinza hadi Magomeni bila ya kupata usumbufu wowote na maisha yake yote sasa hivi asilimia kubwa anatembea kwa miguu.