FIFA yamfungia Eto'o
BREAKING NEWS: ET'OO AFUNGIWA
Shirikisho la Soka Duniani FIFA limefungia miezi 6 Rais wa Shirikisho la soka nchini Cameroon (FECAFOOT) Samuel Eto'o kutohudhuria michezo yeyote ya timu ya Taifa hilo.
Eto'o, ambaye ni Rais wa Shirikisho la kandanda nchini Cameroon tangu 2021, alikabiliwa na mashtaka mawili kutokana na tukio la Kombe la Dunia la Wanawake chini ya miaka 20 nchini Colombia Septemba 11.
Kwa mujibu wa kamati ya nidhamu ya FIFA, Eto’o alipatikana kuwa alikiuka vifungu vya 13 (“tabia ya kukera na ukiukaji wa kanuni za uchezaji wa haki”) na 14 (“Utovu wa nidhamu wa wachezaji na viongozi”) ya kanuni za nidhamu za FIFA.