KenGold kufanya sherehe ya kufungwa goli moja na Yanga
Taarifa iliyopo kwasasa kwamba klabu ya KenGold ya Chunya mkoani Mbeya inataka kufanya sherehe kubwa baada ya kufungwa goli moja na Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uliochezwa jana.
Msemaji wa timu hiyo Jobe Mkoko ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.
"Kuna watu walianzishwa 1936 lakini walipigwa 7 na Yanga,wengine juzi tu walikufa 6.Sisi kama KENGOLD tutafanya sherehe kufungwa goli moja tu na YangaSc"