Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2024

TWENTY PARCENT KUREJEA TENA KWENYE BONGO FLEVA

Picha
Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Twety Parcent ameongea kuhusu ujio wake kwenye industry ya Bongo fleva na kuongelea baadhi ya vitu. Twenty Percent ameeleza kuhusu mabadiliko ya muziki wa Bongo Fleva na kueleza kuwa kwa sasa hakuna wana muziki wa wasanii Tanzania bali kuna Wana Riziki. Twenty ameongeza kuwa wengi sio wasanii ila wana force kuishi maisha ya kisanii na ndio mana unasikia watu wengi wakihoji juu ya maisha ya msanii flani mfano gari analotembelea badala ya kuhoji kuhusu muziki wake. Ameongeza kuwa anashamgazwa sana na wasanii wanaoingia studio kila siku kurekodi na hao ndio wanaoharibu muziki kwa sababu wanaharibu misingi wa muziki. Pia ameongelea suala la tuzo zilivyoharibiwa baada ya watu kuanza kupeana tuzo kwa kufahamiana.

GAMONDI AMJIA JUU MWANDISHI WA HABARI KWA SWALI LA KISHABIKI

Picha
Kocha wa Yanga Miguel Gamondi amegeuka mbogo kwa Mwandishi wa habari aliyeuliza kwanini amemuazisha kijana Mdogo Mzize na kumuacha Joseph Guede mkomavi na mwenye uzoefu na Michuano mikubwa, wakati wa mkutanao wa Waandishi wa habari baada ya mchezo. "Mzize ni 'Future' ya Tanzania sio Yanga tu, sasa atapataje uzoefu kama hapati nafasi ya kucheza, mbona kacheza vizuri sana, katengeneza nafasi nyingi, kukosa ni kawaida kwa washambuliaji, au hujaona alichokifanya, wewe ni mwandishi wa habari nadhana una uelewa wa mambo kuliko shabiki, sasa unaulizaje swali kama shabiki, aya nami nikuulize yule Peter Shelulile wa Mamelod Sundowns katengeneza nafasi ngapi?" -

YANGA YAVUNJA REKODI KWA MKAPA

Picha
Kwa mara ya kwanza uwanja wa Benjamin Mkapa ulijaa na waliojaza huo uwanja si wengine bali ni mashabiki wa Yanga mashabiki elfu sitini 60000 hadi Azam TV waliwataarifu mashabiki waliopo nje ya uwanja warudi nyumbani wafuatilie mchezo kupitia televisheni uwanjani hakuna nafasi ya kukaa Kwa maana hiyo Yanga imeweka rekodi kwa kujaza mashabiki wengi kuliko timu yoyote hapa nchini iliyoweza kujaza mashabiki wengi #𝗗𝘂𝗸𝗲𝘂𝗽𝗱𝗮𝘁𝗲𝘀

AZAM FC KUMSHUSHA MRITHI WA PRINCE DUBE

Picha
Klabu ya Azam FC ipo kwenye mazungumzo ya kumsajili Mshambuliaji raia wa Uganda Sadat Anaku (23) kutoka Dundee FCX Anaku alijiunga na timu ya Scotland mwaka 2022 baada ya kufanya vyema katika ligi kuu ya Uganda akiwa na KCCA FC lakini hakuwa na bahati nzuri kutokana na majeraha yakiyokuwa yakimuandama na kupelekea kukosa muda mwingi wa kuitumikia klab hiyo, Mkataba wa Anaku na timu ya Scotland unamalizika mwishoni mwa msimu huu na mpaka sasa hakuna mazungumzo ya kuongezwa kwa mkataba wake, Azam Fc wanapewa kipaumbele zaidi na hii ni baada ya Uongozi wa mchezaji huyo kuridhishwa na Miundo mbinu na mazingira yote ya kuishi kwa Mshambuliaji huyo. .

TUNGEFUNGUKA TUNGEFUNGWA MENGI- GAMONDI

Picha
Kocha wa Yanga Miguel Gamondi raia wa Argentina amesema timu yake isingeweza kufunguka na kushambulia kwa kasi kwani wamgefanya hivyo kuna uwezekano mkubwa wangefungwa idadi kubwa ya mabao. "Huwezi kucheza na Mamelod ukafunguka hovyo,walimiliki mpira lakini hawakuwa na madhara yoyote,tumetengeneza nafasi za kumaliza. Mechi, hatukupata goli. Mimi napenda kucheza mpira lakini ukicheza na Mamelod huwezi kupishana nao lazima uende na mbinu na ndicho tumefanya Leo" "Wachezaji wangu wamecheza vizuri , hazikuwa dakika 90 nyepesi lakini tumepambana kwa kadri ya uwezo wetu. Mechi kubwa hii mwisho wa siku tuna dakika nyingine 90 ugenini" Alisema Gamondi kocha wa Yanga SC

UCHAMBUZI WA PRIVADINHO KUHUSU MECHI YA YANGA NA MAMELODI

Picha
Mamelodi leo walionesha kitu ambacho mara nyingi wanakionesha Brighton ( kwenye build up ) kipi hiko ?Kukuvuta uende kuwafanyia pressing ( Baiting the press ) na kwanini hivyo ? 1: Ni kwamba wanapasiana taratibu nyuma pasi fupi fupi dhamira yao uende ukawafanyie pressing ili space ifunguke nyuma yako washambulie nyuma ya kiungo chako , pasi mbili au tatu wanakusalimia 2: Wanakuwa mabeki wawili nyuma , viungo wawili mbele yao huku fullbacks wakiwa wanatanua uwanja kwenye mstari wa mmoja na viungo wawili , huku GK anakuwa kama option ya ziada wakitaka pasi ya mbele Lakini Yanga wao wakasema " No thank you " huo mpira kaeni nao huko kwenu hatuji kufanya pressing , Yanga walitengeneza midblock nzuri ya 4-4-2 ( walikabia katikati zaidi na wala sio chini wala juu sana ) kuwanyima space za ndani ya Mamelodi jumlisha kazi nzuri ya Maxi na Musonda kwenye ku track back kuhakikisha fullbacks wao wasiwe wazi peke yao . Game Plan Kwa kipindi cha kwanza tu pekee ilihitaji hivi vitu viwili ...

YANGA YAIVIMBIA MAMELODI

Picha
Na Shafih Matuwa Wawakilishi wengine was Tanzania katika michuano ya kimataifa Yanga SC usiku huu wameilazimisha sare 0-0 Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya mwbingwa Afrika katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Mchezo uliokuwa mkali na mgumu ambapo timu zote zilifanya mashambulizi kwa zamu, Yanga leo imewakosa wachezaji wake tegemeo watatu Pacome Zouzoua, YKouassi Yao wote raia wa Ivory Coast na Khalid Aucho. Kwa matokeo hayo sasa Yanga inahitaji sare ya mabao ili iweze kusonga mbele huku Mamelodi wanatakiwa kushinda kwa njia yoyote

MBWANA SAMATTA KUANZISHA TELEVISHENI YAKE

Picha
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta yuko mbioni kuanzisha televisheni yake. Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa mshambuliaji huyo wa Paoko ya Ugiriki ambaye pia amepata kucheza katika vilabu vya TP Mazembe ya DR Congo, KRC Genk ya Ubelgiji, Aston Villa ya Uingereza na Fernebahce ya Uturuki. Samatta anataka kuweka heshima kwa kufungua televisheni yake ambayo itabamba Afrika nzima na dunia kwa ujumla, pia mtoa taarifa huyo amedai Samatta anahusika kwa kiasi kikubwa uanzishwaji wa redio ya Ali Kiba iitwayo Crown FM ambapo Inasemekana wataimiliki wote

MAJERUHI WA AJALI YA MASHABIKI WA SIMBA WAENDELEA VIZURI

Picha
Wagonjwa waliopata ajali juzi wakati wakija kuushuhudia mchezo wa Ligi ya mabingwa. Afrika kati ya Simba SC na Al Ahly uliochezwa jana kwenye uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam wanaendelea vizuri. Wagonjwa hao ni mashabiki wa klabu ya Simba waliotokea mkoani Mbeya walipata ajali mkoani Pwani na kusababisha watu wawili kufariki dunia na wengine kadhaa kupatwa ma majeraha

BEKI WA KATI MAMELODI KUTIMKA

Picha
Beki Kati wa Kimataifa wa Kenya, Brian Mandela Onyango Mwenye umri wa miaka (29) anatarajia Kuondoka katika Klabu yake ya Mamelodi Sundowns ya Afrika kusini, baada ya kumalizika msimu huu Baada ya Kuhudumu katika klabu hiyo kwa Muda wa Miaka Mitano. Brian Mandela Alijiunga na Masandawana mwaka 2020 akitokea Klabu ya Maritzburg United na Alisaini Mkataba wa miaka Mitano unaofikia tamati mwishoni mwa msimu huu, Akiwa na Sundowns Mandela ametwaa mataji Matatu ya ligi na Vikombe vingine vitatu ikiwemo AFL ya msimu huu.

AL AHLY YAICHINJA SIMBA NYUMBANI

Picha
Timu ya Al Ahly ya Misri usiku huu imeifu ga Simba SC ya Tanzania bao 1-0 katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam mchezo wa robo fainali Ligi ya mabingwa Afrika. Kwa matokeo ya mchezo huo, Simba sasa inatakiwa kushinda zaidi ya bao moja pasipo kiruhusu bao ili iweze kutinga nusu fainali. Bao lililoizamisha Simba mbele ya mashabiki wake lilifungwa na Ahmed Kouka dakika ya 5 kipindi cha Kwanza. Kesho katika uwanja huo huo Yanga wataikaribisha Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini hatua ya robo fainali

FISTON MAYELE KUREJEA YANGA

Picha
Na Imram Khamees Meneja wa Mshambuliaji kutoka DR Congo na Klabu ya Pyramids ya Misri, Fiston Kalala Mayele aliyemleta Tanzania Nestor Mutuale, amesema kuwa mchezaji huyo bado anaiheshimu sana klabu yake ya zamani ya Yanga SC ambayo imemuweka kwenye ramani ya soka la ushindani Kimataifa. Kauli hiyo ya Mutuale inakuja baada ya vyombo vya habari nchini Tanzania kuripoti kuwa mshambuliaji huyo aliyefanya makubwa kwa misimu miwili mfulululizo na Wananchi wa Jangwanai anataka kuhamia Azam Fc na Wengine wakisema Simba SC baada ya kushindwa kufanya vizuri nchini Misri, “Mteja wangu anajua vizuri thamani na jukwaa ambalo Young Africans walimpatia kama itabidi kurudi Tanzania basi nafasi ya kwanza watapewa Young Africans Ila kwa sasa ana furaha ndani ya Pyramid labda mengine yatokee mbele lakini kwa sasa yuko na furaha,” amesema meneja wa Mayele. Yanga wanatajwa kufikia makubaliano mazuri na aliyekuwa mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube baada ya kutemana na matajiri hao wa Dar es Salaam.FISTON...

AZIZ KI, DIARRA WASHUSHA PRESHA YANGA

Picha
Golikipa Namba moja wa Klabu ya Yanga, Djigui Diarra na Kiungo Mshambuliaji Stephen Aziz Ki wamerejea nchini na jioni ya leo na moja moja wameingia kambini Avic Town. Wachezaji hao Jioni hii wamefanya mazoezi na wachezaji wenzao tayari kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo wa kesho Jumamosi wa hatua ya Robo Fainali dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika KusiniKatika Michuano ya Ligi Mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowans ya Afrika Kusini.

CHANUO BADO NI MKE WANGU- MADEBE

Picha
Staa wa Michezo ya kuigiza (Bo gomu I) Madebe Lidai amesema msanii mwenzake Chanuo bado ni mke wake tofauti na watu wanavyodai kwamba wameacha a.  "Chanuo bado ni mke wangu, mama watoto wangu na yeye ananitambua kama mume wake, kugombana kupo ukizingatia sisi wote ni maarufu kwahiyo lazima matatizo yetu yawachanganye watu. I la kwa sasa tuko sawa hayo mengine yaliyonikuta ni sehemu ya uanaume tu misukosuko ni lazima" - Madebe Lidai

CEO SIMBA SC ASEMA GOLI 5 WALIZOPIGWA NA YANGA ILIKUWA BAHATI TU

Picha
Hivi karibuni yalosikika maneno ya msemaji wa serikali kuhusu tamko lililowahi kutolewa na waziri wa Michezo  sanaa na Utamaduni Dkt Damas Ndumbaro kuhusu kuwataka mashabiki wa soka kuingia uwanjani kushuhudia mechi za Al Ahly na Simba au Mamelodi na Yanga waende wakiwa na pasipoti. Lakini msemaji huyo wa serikali akaibuka na kudai waziri Ndumbaro alifanya utani tu, hivyo ndio kama CEO wa klabu ya Simba Imani Kajula ambapo anasema kipigo ilichokipata Simba ilipocheza na Yanga cha mabao 5-1 ni kama bahati tu Yanga iliipata. "Haya ni mafanikio ya timu tu kuingia hatua Robo fainali katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika ile Yanga kutufunga magoli 5, Yanga walibahatisha" "Kitu kisichokuwa na thamani kinakuwa bure, Unapofanya mzunguko bure unainyima Serikali asilimia 15 ya mapato" Imani Kajula - Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba akiongea kupitia kituo cha Efm radio. Kajula

MASHABIKI WAWILI SIMBA WAFA AJALINI

Picha
Watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha na wengine 29 kujeruhiwa, katika ajali ya basi dogo aina ya Coaster lililobeba mashabiki wa Klabu ya Simba wa Tawi la Ibirilo Junction kutoka Rungwe, Mbeya kupata ajali mapema alfajiri ya leo eneo la Vigwaza. Mashabiki hao walikuwa wakija Dar es Salaam ambapo leo klabu hiyo ina mchezo wa robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri. Kamanda wa Polisi Pwani ameahidi kutoa taarifa zaidi baadaye.

AISHI MANULA NDIO BASI TENA

Picha
Golikipa wa klabu ya Simba SC na timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" Aishi Manula ataendelea kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu zaidi Kati ya miezi kumi (10) hadi Miezi (12) kutokana na majeraha yanayomkabili aliyoyapata akiwa katika majukumu ya Timu Taifa Nchini Azerbaijan. Manula alipata jeraha linalofanana na jeraha la mwisho ambalo lilimuweka nje kwa muda mrefu zaidi ya Miezi sita (6), Manula Atakosa Mchezo wa Leo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly na Golikipa Ayoub Lakred atasimama langoni katika Mchezo huo muhimu. Katika Hatua Nyingine Klabu ya Simba Itakosa Huduma ya nyota wake Wengine watatu, Ambao ni Ladack Chasambi, Edwin Balua na Salehe Karabaka ambao awakufanya Mazoezi ya mwisho siku ya Jana Kuelekea katika Mchezo wa leo Dhidi ya Al Ahly, huku Sababu ikiwa ni kutokuwa katika Mipango ya Kocha Abdelahak Benchikah Kuelekea mchezo huo.

KOCHA AL AHLY KUIMALIZA MECHI MAPEMA KESHO

Picha
Kocha Mkuu wa Klabu ya Al Ahly SC Marcel Koller ameahidi kuimaliza mechi yao dhidi ya Simba SC Siku ya Kesho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na hajali kuhusu rekodi ya michezo ya nyuma baina yao dhidi ya Simba SC Walipokutana ambapo hawakuwa na Matokeo mazuri. “Tumejiandaa vyema kuonesha kiwango bora kesho na tunakwenda kushinda kwa kuwa hatujaja kuangalia historia yetu na yao bali kucheza mpira, Hatutacheza kwa ajili ya kusubiri kuumaliza mchezo nyumbani , tutacheza kwa umakini kwa nia ya kuumaliza Mchezo hapa hapa ugenini “ “Nimecheza nao Simba mechi mbili (2) na msimu huu na Mechi zote tumetoa sare, niliwaona na naweza kusema kuwa wapo kwenye level kama yetu siyo wadogo kwa hiyo hatutawadharau hata Kidogo tutaingia kwenye mchezo wa Kesho kwa nguvu zote kutafuta matokeo na si vinginevyo.” Alisema Marcel Koller Kocha Mkuu Wa Al Ahly Kocha wa Al Ahly

BENCHIKHA AAHIDI KUIFIKISHA SIMBA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Picha
Akiongea Kwenye mkutano na waandishi wa habari Kuelekea Mchezo wa Kesho wa Robo Fainali ya kwanza dhidi ya Al Ahly ya Egypt, Kocha mkuu wa Simba SC ametoa ahadi ya kuipeleka Simba SC katika hatua ya Nusu Fainali msimu huu kwa kuwatoa Al Ahly SC. “Nataka kuivusha Simba Robo fainali na kwenda Nusu fainali, hayo ni malengo yangu hadi wachezaji, nataka tuende mbele zaidi tofauti na ambapo Simba huwa inafikia, safari hii nataka kuivusha Simba na najua wachezaji wangu wapo tayari” “Hakuna kitu kigumu katika mpira, sisi Simba tunaenda kupigana kwenye hatua hii kuanzia nyumbani hadi ugenini, kikubwa mashabiki wetu kuwa na imani na sisi na kujitokeza kwa wingi uwanjani” Abdelhak Benchikha

VINARA WA MAGOLI LIGI YA MABINGWA AFRIKA, PACOME NDANI

Picha
Na Van Mapande Orodha ya Wachezaji (5) Vinara wa Magoli Katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF Champions League) mpaka Sasa huku Kinara akiwa Mshambuliaji Sankara Karamoko ambaye alishatimka katika Klabu ya ASEC Mimosas katika dirisha la Usajili la mwezi January na Kujiunga na Klabu ya Wolfsberger AC ya Austria. 1. Sankara Karamoko(Asec) - 5️⃣ 2. Pacome Zouzoua(Yanga) - 4️⃣ 3. Saido Ntibanzonkiza (Simba) - 4️⃣ 4. Fiston Mayele(Pyramids) - 3️⃣ 5. Glody Likonza(Mazembe) -3️⃣

MWAMNYETO AIGOMEA YANGA

Picha
Nahodha wa Yanga SC Bakari Nondo Mwamnyeto amegoma kurejea kambini kujiandaa na mchezo wa robo fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika CAFCL dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini  kutoķana na kile kinachodaiwa ufinyu wa nafasi katika kikosi cha kwanza. Katika mechi za hivi karibuni kocha wa Yanga Miguel Gamondi amekua akiwatumia Dickson Job na Ibrahim Baka kama mabeki wakati, kitu ambacho kinamnyima furaha Mwamnyeto

TBC KUZITANGAZA MECHI ZA ROBO FAINALI SIMBA, YANGA

Picha
Shirika la Utangazaji Tanzania TBC litaonyesha Michezo ya Robo Fainali ya Klabu Bingwa Barani Afrika kati ya Simba SC Dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Kesho Ijumaa na Mchezo wa Yanga SC Dhidi ya Mamelodi Sundown siku ya Jumamosi Michezo yote Hiyo Itaruka Mubashara Kupitia TBC1 Bure kwa Muonekano wa Picha ang'avu yaani FULL HD #FutbalPlanetUpdates KUTOKA TBC. Shirika la Utangazaji Tanzania TBC litaonyesha Michezo ya Robo Fainali ya Klabu Bingwa Barani Afrika kati ya Simba SC Dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Kesho Ijumaa na Mchezo wa Yanga SC Dhidi ya Mamelodi Sundown siku ya Jumamosi Michezo yote Hiyo Itaruka Mubashara Kupitia TBC1 Bure kwa Muonekano wa Picha ang'avu yaani FULL HD

SIMBA YATOA MSAADA KWA WATOTO WA KURASINI

Picha
Klabu ya Simba kwa kushirikiana na wanachama imetoa misaada kwenye Makazi ya Watoto yaliyopo Kurasini, Dar es Salaam. Simba imeamua kutoa misaada kwa watoto hao ikielekea kwenye mchezo wake wa robo fainali dhidi ya Al Ahly utakaofanyika kesho kwenye uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Lakini pia Imetoa msaada huo katika kipindi hiki cha mfungo wa Kwaresma na Ramadhan ikiwa na kauli mbiu "Mechi ni mashabiki"

BABA YAKE HAJI MANARA AMJIA JUU KADUGUDA

Picha
Mchezaji wa zamani wa Yanga SC na Taifa Stars, Sunday Manara, amesikitishwa na kauli iliyotolewa siku chache zilizopita na Mjumbe wa Bodi ya Wakuregenzi ya Simba, Mwina Seif Kaduguda 'Simba wa Yuda' juu ya viwango vya baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo. Kaduguda alisema, wachezaji wa kimataifa waliosajiliwa na Simba SC ni wabovu hata ukienda Buguruni, Mwananyamala na Temeke wamejaa wenye uwezo kama wao. Sunday Manara kupitia kipindi cha michezo cha The Scoreboard ya Times FM, alisema kauli hiyo ni ya kupingwa vikali kwa kuwa inachafua dira ya mpira wetu ambao unaonekana kupiga hatua kwa haraka sana. Aidha amemshauri kiongozi huyo atumie njia sahihi za kushauri hususani katika vikao vyao vya ndani na sio kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kama alivyofanya, kufanya hivyo ni kama kutafuta umaarufu mitandaoni.

TIMU YA MAXI NZENGELI YAVUNJA PAMBANO DR CONGO

Picha
Katika mchezo wa ligi kuu nchibi DR Congo kati ya Maniema dhidi ya Lupopo, ambapo mashabiki wa klabu ya Maniema walimpiga mwamuzi aliyekuwa anachezeha mchezo huo baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya mwamuzi huo. Maniema ndiyo timu aliyokuwa anaichezea kiungo mshambuliaji wa Yanga, Maxi Nzengeli wakati Lupopo ni timu anayouchezea George Mpole aliyewahi kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu bara msimu wa 2022/2023

KOPUNOVIC HUYOO COASTAL UNION

Picha
Aliyekuwa kocha wa Tabora Jnited Goran Kopunovic yupo mbioni kujiunga na Coastal Union. Kwa sasa yupo kwenye hatua za mwisho kumalizana nao, Coastal malengo yao ni kumaliza nafasi ya 4 ili wacheze michuano ya kimataifa msimu ujao Goran Kopunovic

VAR KWA MKAPA IMEELEWEKA

Picha
Mifumo ya Video Assistant Referee (VAR) tayari umeanza kufungwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa Nchini Tanzania. Video Assistant Referee (VAR) itatumika kwenye michezo yote ya Robo fainali ya CAF.

AL AHLY WALIVYOWASILI DAR ES SALAAM KINYONGE

Picha
Klabu ya Al Ahly imewasili Tanzania kwa ajili ya mchezo wa hatua ya robo fainali ya CAFCL dhidi ya Simba SC, Ijumaa katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Hii ni mara ya pili kwa Simba na Al Ahly kukutana msimu huu, mara yao ya kwanza ilikuwa kwenye michuano ya African Football League (AFL) ambapo zilifungana 3-3, yaani 2-2 jijini Dar es Salaam na 1-1 jijini Cairo

ONANA ASEMA HUU NDIO MWAKA WA SIMBA KUTINGA NUSU FAINALI

Picha
Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Cameroon na Simba SC, Willy Onana, amesema huu ndiyo wakati muhimu kwa timu yake kwenda kuandika historia mpya Barani Afrika kwa kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa mara ya kwanza. “Binafsi najisikia vizuri kucheza Robo Fainali kwa mara ya kwanza, Al Ahly ni kama Real Madrid kwa Afrika inaweza kuwa katika kipindi cha mpito lakini katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wanakuja kivingine. Tunatambua tunakwenda kucheza na timu kubwa sana barani Afrika, hizi ni nyakati bora kwa wachezaji na viongozi wa Benchi la Ufundi kuandika historia mpya,” Amesema kama kuna aliyekuwa akiingalia Simba SC ikiishia hatua ya Robo Fainali abadilishe mtazamo kwa kuwa huu ni wakati wa kwenda kubadili hii historia ambayo kwa muda mrefu wamekuwa wakiisubiri. “Sijui mipango ya mwalimu katika mchezo huo lakini mimi binafsi niko tayari kwa ajili ya mechi hii kubwa ambayo itatazamwa na watu wengi Barani Afrika,” amesema Onana. Simba SC imefika hatua hiyo baada ...

TABORA UNITED KWABOMOKA

Picha
Ofisa Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa Klabu ya Tabora United Thabit Kandoro ameomba kujiuzulu kwa kutoendelea na majukumu katika nafasi yake ya Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo kuanzia leo Jumatano Machi 27, baada ya kutoridhishwa na mambo yanavyoendeshwa ndani ya timu hiyo ambapo mambo mengi yanaonekana kutokuwa katika mpangilio mzuri wa kufanya kazi. Ripoti kutoka Mkoani Tabora Zimeeleza kuwa Kandoro ameshawasilisha barua tayari kwa waajiri wake, anaisubiri majibu yao kwasasa, Ikumbukwe Thabit Kandoro alishawahi kufanya kazi Yanga SC, kama mkurugenzi wa mashindano na usajili pia Aliwahi kuhudumu katika Kituo cha Fountain Gate Academy cha Jijini Dodoma. Pia katika hatua nyingine baadhi ya Wachezaji wa klabu hiyo wamegoma kurejea kambini ndani ya klabu hiyo Kutokana Changamoto mbali mbali wanazozipitia tangu walipojiunga na timu hiyo ikiwemo suala l a madai ya pesa za Usajili na mishahara walionayo dhidi ya Klabu hiyo kutokea mkoani Tabora

SIMBA INA KILA SABABU YA KUITOA AL AHLY

Picha
Na Prince Hoza MWISHO wa Al Ahly umefika naweza kusema hivyo, mpira umebadilika sana hapa Afrika na tumejionea kwenye michuano iliyomalizika ya mataifa Afrika, AFCON iliyofanyika nchini Ivory Coast ambapo timu maarufu ziliambulia patupu.  Lakini pia michuano hiyo tumeshuhudia miamba ya kutoka Afrika kaskazini, kwa maana timu za Kiarabu kuondoshwa mapema, mataifa makubwa kama ya Morocco, Algeria, Tunisia na Misri zilishindwa kupenya.  Kushindwa kwa mataifa hayo, kulizifanya mataifa yasiyo na umaarufu kuibuka, hivyo ndivyo ilivyo kwa upande wa vilabu katika michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika na kombe la Shirikisho.  Katika Ligi ya mabingwa, safari hii mataifa ya Waarabu hayajafua dafu na kujikuta yakiondoshwa mapema, Al Ahly na Esperance ya Tunisia ndio timu pekee zilizofanikiwa kuingia robo fainali, na mwenendo wao si mzuri. Vilabu kama vya Pyramids ya Misri, Wydad Casablanca ya Morocco na CR Belouizdad ya Algeria ziliishia makundi.  Sio kawaida kwa mataifa ya kiarabu kuondoshwa mapema...