TUNGEFUNGUKA TUNGEFUNGWA MENGI- GAMONDI

Kocha wa Yanga Miguel Gamondi raia wa Argentina amesema timu yake isingeweza kufunguka na kushambulia kwa kasi kwani wamgefanya hivyo kuna uwezekano mkubwa wangefungwa idadi kubwa ya mabao.

"Huwezi kucheza na Mamelod ukafunguka hovyo,walimiliki mpira lakini hawakuwa na madhara yoyote,tumetengeneza nafasi za kumaliza.

Mechi, hatukupata goli. Mimi napenda kucheza mpira lakini ukicheza na Mamelod huwezi kupishana nao lazima uende na mbinu na ndicho tumefanya Leo"

"Wachezaji wangu wamecheza vizuri , hazikuwa dakika 90 nyepesi lakini tumepambana kwa kadri ya uwezo wetu. Mechi kubwa hii mwisho wa siku tuna dakika nyingine 90 ugenini"

Alisema Gamondi kocha wa Yanga SC


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA