BENCHIKHA AAHIDI KUIFIKISHA SIMBA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA
Akiongea Kwenye mkutano na waandishi wa habari Kuelekea Mchezo wa Kesho wa Robo Fainali ya kwanza dhidi ya Al Ahly ya Egypt, Kocha mkuu wa Simba SC ametoa ahadi ya kuipeleka Simba SC katika hatua ya Nusu Fainali msimu huu kwa kuwatoa Al Ahly SC.
“Nataka kuivusha Simba Robo fainali na kwenda Nusu fainali, hayo ni malengo yangu hadi wachezaji, nataka tuende mbele zaidi tofauti na ambapo Simba huwa inafikia, safari hii nataka kuivusha Simba na najua wachezaji wangu wapo tayari”
“Hakuna kitu kigumu katika mpira, sisi Simba tunaenda kupigana kwenye hatua hii kuanzia nyumbani hadi ugenini, kikubwa mashabiki wetu kuwa na imani na sisi na kujitokeza kwa wingi uwanjani”