CEO SIMBA SC ASEMA GOLI 5 WALIZOPIGWA NA YANGA ILIKUWA BAHATI TU

Hivi karibuni yalosikika maneno ya msemaji wa serikali kuhusu tamko lililowahi kutolewa na waziri wa Michezo  sanaa na Utamaduni Dkt Damas Ndumbaro kuhusu kuwataka mashabiki wa soka kuingia uwanjani kushuhudia mechi za Al Ahly na Simba au Mamelodi na Yanga waende wakiwa na pasipoti.

Lakini msemaji huyo wa serikali akaibuka na kudai waziri Ndumbaro alifanya utani tu, hivyo ndio kama CEO wa klabu ya Simba Imani Kajula ambapo anasema kipigo ilichokipata Simba ilipocheza na Yanga cha mabao 5-1 ni kama bahati tu Yanga iliipata.

"Haya ni mafanikio ya timu tu kuingia hatua Robo fainali katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika ile Yanga kutufunga magoli 5, Yanga walibahatisha"

"Kitu kisichokuwa na thamani kinakuwa bure, Unapofanya mzunguko bure unainyima Serikali asilimia 15 ya mapato"

Imani Kajula - Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba akiongea kupitia kituo cha Efm radio.

Kajula

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA