SIMBA YATOA MSAADA KWA WATOTO WA KURASINI
Klabu ya Simba kwa kushirikiana na wanachama imetoa misaada kwenye Makazi ya Watoto yaliyopo Kurasini, Dar es Salaam.
Simba imeamua kutoa misaada kwa watoto hao ikielekea kwenye mchezo wake wa robo fainali dhidi ya Al Ahly utakaofanyika kesho kwenye uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Lakini pia Imetoa msaada huo katika kipindi hiki cha mfungo wa Kwaresma na Ramadhan ikiwa na kauli mbiu "Mechi ni mashabiki"