MAJERUHI WA AJALI YA MASHABIKI WA SIMBA WAENDELEA VIZURI
Wagonjwa waliopata ajali juzi wakati wakija kuushuhudia mchezo wa Ligi ya mabingwa. Afrika kati ya Simba SC na Al Ahly uliochezwa jana kwenye uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam wanaendelea vizuri.
Wagonjwa hao ni mashabiki wa klabu ya Simba waliotokea mkoani Mbeya walipata ajali mkoani Pwani na kusababisha watu wawili kufariki dunia na wengine kadhaa kupatwa ma majeraha