AL AHLY WALIVYOWASILI DAR ES SALAAM KINYONGE
Klabu ya Al Ahly imewasili Tanzania kwa ajili ya mchezo wa hatua ya robo fainali ya CAFCL dhidi ya Simba SC, Ijumaa katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Hii ni mara ya pili kwa Simba na Al Ahly kukutana msimu huu, mara yao ya kwanza ilikuwa kwenye michuano ya African Football League (AFL) ambapo zilifungana 3-3, yaani 2-2 jijini Dar es Salaam na 1-1 jijini Cairo