UCHAMBUZI WA PRIVADINHO KUHUSU MECHI YA YANGA NA MAMELODI


Mamelodi leo walionesha kitu ambacho mara nyingi wanakionesha Brighton ( kwenye build up ) kipi hiko ?Kukuvuta uende kuwafanyia pressing ( Baiting the press ) na kwanini hivyo ?

1: Ni kwamba wanapasiana taratibu nyuma pasi fupi fupi dhamira yao uende ukawafanyie pressing ili space ifunguke nyuma yako washambulie nyuma ya kiungo chako , pasi mbili au tatu wanakusalimia

2: Wanakuwa mabeki wawili nyuma , viungo wawili mbele yao huku fullbacks wakiwa wanatanua uwanja kwenye mstari wa mmoja na viungo wawili , huku GK anakuwa kama option ya ziada wakitaka pasi ya mbele

Lakini Yanga wao wakasema " No thank you " huo mpira kaeni nao huko kwenu hatuji kufanya pressing , Yanga walitengeneza midblock nzuri ya 4-4-2 ( walikabia katikati zaidi na wala sio chini wala juu sana ) kuwanyima space za ndani ya Mamelodi jumlisha kazi nzuri ya Maxi na Musonda kwenye ku track back kuhakikisha fullbacks wao wasiwe wazi peke yao . Game Plan

Kwa kipindi cha kwanza tu pekee ilihitaji hivi vitu viwili goli lipatikane

1: Makosa makubwa ya kiulinzi kwa timu zote mbili
2: Ubora wa mchezaji mmoja kuamua ( individual brilliance )

Kipindi cha pili kuna muda kama wa dakika 20 au 15 fulani hivi , timu zote mbili ziliamua kufunguka na kupishana hapo spaces zilianza kufunguka , runners wakaanza kupata spaces , pasi za mbele zilianza kuonekana , kilichokosekana :-

1: Mamelodi pasi yao ya mwisho ilikosekana
2: Yanga maamuzi sahihi , either pasi au umaliziaji

kwenye uzuiaji timu zote zilikuwa tofauti kwenye muundo wao

Mamelodi walichagua kukabia juu hasa pale wakipoteza mpira ( counter pressing )

Yanga kufunga spaces wakiwa ndani : na wote ( Mamelodi na Yanga walifanikiwa kwenye mipango yao )


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI