MASHABIKI WAWILI SIMBA WAFA AJALINI
Watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha na wengine 29 kujeruhiwa, katika ajali ya basi dogo aina ya Coaster lililobeba mashabiki wa Klabu ya Simba wa Tawi la Ibirilo Junction kutoka Rungwe, Mbeya kupata ajali mapema alfajiri ya leo eneo la Vigwaza.
Mashabiki hao walikuwa wakija Dar es Salaam ambapo leo klabu hiyo ina mchezo wa robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri.
Kamanda wa Polisi Pwani ameahidi kutoa taarifa zaidi baadaye.