BEKI WA KATI MAMELODI KUTIMKA
Beki Kati wa Kimataifa wa Kenya, Brian Mandela Onyango Mwenye umri wa miaka (29) anatarajia Kuondoka katika Klabu yake ya Mamelodi Sundowns ya Afrika kusini, baada ya kumalizika msimu huu Baada ya Kuhudumu katika klabu hiyo kwa Muda wa Miaka Mitano.
Brian Mandela Alijiunga na Masandawana mwaka 2020 akitokea Klabu ya Maritzburg United na Alisaini Mkataba wa miaka Mitano unaofikia tamati mwishoni mwa msimu huu, Akiwa na Sundowns Mandela ametwaa mataji Matatu ya ligi na Vikombe vingine vitatu ikiwemo AFL ya msimu huu.