AZAM FC KUMSHUSHA MRITHI WA PRINCE DUBE
Klabu ya Azam FC ipo kwenye mazungumzo ya kumsajili Mshambuliaji raia wa Uganda Sadat Anaku (23) kutoka Dundee FCX
Anaku alijiunga na timu ya Scotland mwaka 2022 baada ya kufanya vyema katika ligi kuu ya Uganda akiwa na KCCA FC lakini hakuwa na bahati nzuri kutokana na majeraha yakiyokuwa yakimuandama na kupelekea kukosa muda mwingi wa kuitumikia klab hiyo,
Mkataba wa Anaku na timu ya Scotland unamalizika mwishoni mwa msimu huu na mpaka sasa hakuna mazungumzo ya kuongezwa kwa mkataba wake,
Azam Fc wanapewa kipaumbele zaidi na hii ni baada ya Uongozi wa mchezaji huyo kuridhishwa na Miundo mbinu na mazingira yote ya kuishi kwa Mshambuliaji huyo.