KOCHA AL AHLY KUIMALIZA MECHI MAPEMA KESHO

Kocha Mkuu wa Klabu ya Al Ahly SC Marcel Koller ameahidi kuimaliza mechi yao dhidi ya Simba SC Siku ya Kesho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na hajali kuhusu rekodi ya michezo ya nyuma baina yao dhidi ya Simba SC Walipokutana ambapo hawakuwa na Matokeo mazuri.

“Tumejiandaa vyema kuonesha kiwango bora kesho na tunakwenda kushinda kwa kuwa hatujaja kuangalia historia yetu na yao bali kucheza mpira, Hatutacheza kwa ajili ya kusubiri kuumaliza mchezo nyumbani , tutacheza kwa umakini kwa nia ya kuumaliza Mchezo hapa hapa ugenini “

“Nimecheza nao Simba mechi mbili (2) na msimu huu na Mechi zote tumetoa sare, niliwaona na naweza kusema kuwa wapo kwenye level kama yetu siyo wadogo kwa hiyo hatutawadharau hata Kidogo tutaingia kwenye mchezo wa Kesho kwa nguvu zote kutafuta matokeo na si vinginevyo.”

Alisema Marcel Koller
Kocha Mkuu Wa Al Ahly

Kocha wa Al Ahly


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA