TABORA UNITED KWABOMOKA
Ofisa Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa Klabu ya Tabora United Thabit Kandoro ameomba kujiuzulu kwa kutoendelea na majukumu katika nafasi yake ya Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo kuanzia leo Jumatano Machi 27, baada ya kutoridhishwa na mambo yanavyoendeshwa ndani ya timu hiyo ambapo mambo mengi yanaonekana kutokuwa katika mpangilio mzuri wa kufanya kazi.
Ripoti kutoka Mkoani Tabora Zimeeleza kuwa Kandoro ameshawasilisha barua tayari kwa waajiri wake, anaisubiri majibu yao kwasasa,
Ikumbukwe Thabit Kandoro alishawahi kufanya kazi Yanga SC, kama mkurugenzi wa mashindano na usajili pia Aliwahi kuhudumu katika Kituo cha Fountain Gate Academy cha Jijini Dodoma.
Pia katika hatua nyingine baadhi ya Wachezaji wa klabu hiyo wamegoma kurejea kambini ndani ya klabu hiyo Kutokana Changamoto mbali mbali wanazozipitia tangu walipojiunga na timu hiyo ikiwemo suala l a madai ya pesa za
Usajili na mishahara walionayo dhidi ya Klabu hiyo kutokea mkoani Tabora