YANGA YAIVIMBIA MAMELODI
Na Shafih Matuwa
Wawakilishi wengine was Tanzania katika michuano ya kimataifa Yanga SC usiku huu wameilazimisha sare 0-0 Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya mwbingwa Afrika katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mchezo uliokuwa mkali na mgumu ambapo timu zote zilifanya mashambulizi kwa zamu, Yanga leo imewakosa wachezaji wake tegemeo watatu Pacome Zouzoua, YKouassi Yao wote raia wa Ivory Coast na Khalid Aucho.
Kwa matokeo hayo sasa Yanga inahitaji sare ya mabao ili iweze kusonga mbele huku Mamelodi wanatakiwa kushinda kwa njia yoyote