AL AHLY YAICHINJA SIMBA NYUMBANI
Timu ya Al Ahly ya Misri usiku huu imeifu ga Simba SC ya Tanzania bao 1-0 katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam mchezo wa robo fainali Ligi ya mabingwa Afrika.
Kwa matokeo ya mchezo huo, Simba sasa inatakiwa kushinda zaidi ya bao moja pasipo kiruhusu bao ili iweze kutinga nusu fainali.
Bao lililoizamisha Simba mbele ya mashabiki wake lilifungwa na Ahmed Kouka dakika ya 5 kipindi cha Kwanza.
Kesho katika uwanja huo huo Yanga wataikaribisha Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini hatua ya robo fainali