BABA YAKE HAJI MANARA AMJIA JUU KADUGUDA
Mchezaji wa zamani wa Yanga SC na Taifa Stars, Sunday Manara, amesikitishwa na kauli iliyotolewa siku chache zilizopita na Mjumbe wa Bodi ya Wakuregenzi ya Simba, Mwina Seif Kaduguda 'Simba wa Yuda' juu ya viwango vya baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo.
Kaduguda alisema, wachezaji wa kimataifa waliosajiliwa na Simba SC ni wabovu hata ukienda Buguruni, Mwananyamala na Temeke wamejaa wenye uwezo kama wao.
Sunday Manara kupitia kipindi cha michezo cha The Scoreboard ya Times FM, alisema kauli hiyo ni ya kupingwa vikali kwa kuwa inachafua dira ya mpira wetu ambao unaonekana kupiga hatua kwa haraka sana.
Aidha amemshauri kiongozi huyo atumie njia sahihi za kushauri hususani katika vikao vyao vya ndani na sio kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kama alivyofanya, kufanya hivyo ni kama kutafuta umaarufu mitandaoni.