MBWANA SAMATTA KUANZISHA TELEVISHENI YAKE
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta yuko mbioni kuanzisha televisheni yake.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa mshambuliaji huyo wa Paoko ya Ugiriki ambaye pia amepata kucheza katika vilabu vya TP Mazembe ya DR Congo, KRC Genk ya Ubelgiji, Aston Villa ya Uingereza na Fernebahce ya Uturuki.
Samatta anataka kuweka heshima kwa kufungua televisheni yake ambayo itabamba Afrika nzima na dunia kwa ujumla, pia mtoa taarifa huyo amedai Samatta anahusika kwa kiasi kikubwa uanzishwaji wa redio ya Ali Kiba iitwayo Crown FM ambapo Inasemekana wataimiliki wote