AISHI MANULA NDIO BASI TENA
Golikipa wa klabu ya Simba SC na timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" Aishi Manula ataendelea kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu zaidi Kati ya miezi kumi (10) hadi Miezi (12) kutokana na majeraha yanayomkabili aliyoyapata akiwa katika majukumu ya Timu Taifa Nchini Azerbaijan.
Manula alipata jeraha linalofanana na jeraha la mwisho ambalo lilimuweka nje kwa muda mrefu zaidi ya Miezi sita (6), Manula Atakosa Mchezo wa Leo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly na Golikipa Ayoub Lakred atasimama langoni katika Mchezo huo muhimu.
Katika Hatua Nyingine Klabu ya Simba Itakosa Huduma ya nyota wake Wengine watatu, Ambao ni Ladack Chasambi, Edwin Balua na Salehe Karabaka ambao awakufanya Mazoezi ya mwisho siku ya Jana Kuelekea katika Mchezo wa leo Dhidi ya Al Ahly, huku Sababu ikiwa ni kutokuwa katika Mipango ya Kocha Abdelahak Benchikah Kuelekea mchezo huo.