Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2014

BYE BYE YA HAMOSNOTA YAZIDI KUBAMBA

Picha
Na Regina Mkonde WIMBO mpya wa mwanamuziki chipukizi wa miondoko ya kizazi kipya yaani bongofleva Hashim Momba ukipenda Hamosnota (Pichani ) uitwao Bye bye umeanza kukonga nyoyo na kuanza kujizolea mashabiki ambao wamek,uwa wakimsapoti na kuzidi kubamba na wimbo huo. Msanii huyo aliyejiunga katika tasnia hiyo hivi karibuni amesema huo ni wimbo wake wa kwanza lakini tayari ameshaandaa nyimbo nyingine ila ataziachia muda si mrefu mara ya hii ya Bye bye kufanya vizuri, akizungumza na Mambo Uwanjani Blogspot, Hamosnota ambaye pia huvuma kwa jina la Fujo amedai wimbo huo umemsukuma kuingia kwenye muziki kwa nguvu zote. 'Nimeamua kufanya muziki kutokana na kuwepo ndani ya damu yangu, muziki mimi nimerithi kutoka kwa mababu zangu, zamani babu yangu alikuwa akipiga marimba hivyo mimi nikapata aidia na kuamua kuendeleza kipaji kilichokuwepo ndani ya ukoo wetu', alisema na kuongeza.

AMISSI TAMBWE KUTIMKA RASMI SIMBA LEO

Picha
Mshambuliaji Amisi Tambwe wa Simba anatarajia kuondoka nchini leo kurejea kwao Burundi kwa ajili ya mapumziko huku akiweka wazi kwamba akifika nyumbani atapata jibu la kujiunga na Yanga, Azam FC au kutimkia Uarabuni huku akiweka wazi nia yake ya kutaka kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Afrika ama Kombe la Shirikisho. Akizungumza katika mahojiano maalum jijini Dar es Salaam jana mchana, Tambwe ambaye ni mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2013/14, alisema akiwa nyumbani kwake Burundi, atakuwa na muda mzuri wa kufikiri na kuchagua timu sahihi ya kuichezea msimu ujao.

NI KIAMA LEO: REAL MADRID V BAYERN MUNICH

Picha
Munich , Ujerumani. Mabingwa watetezi Bayern Munich leo watakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha inaichapa Real Madrid wakiwa kwenye uwanja wa wake wa nyumbani ili kujihakikishia kubaki katika mashindano hayo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Miamba hiyo ya Ujerumani haijapoteza mchezo hata mmoja nyumbani katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa msimu huu. Madrid inashuka jijini Munich ikiwa na faida ya ushindi wa bao 1-0, shukrani kwa bao la dakika ya 19 la Karim Benzema kwenye mchezo wa

RAIS WA BRAZIL AMUUNGA MKONO DAN ALVES

Picha
Rais wa Brazil amuunga mkono Alves kwa kula ndizi Swala a tata la ubaguzi wa rangi katika michezo limeibua mchango wa rais wa Brazil. Rais Dilma Rousseff, amesifu kitendo cha mchezaji wa kimataifa wa Brazil, na Barcelona Dani Alves kutokana na tukio la ubaguzi wa rangi wakati wa mechi ya ligi kuu ya Uhispania, La Liga kati ya Barcelona na Villareal .

RATIBA KAMILI YA MATAIFA AFRIKA 2015

Picha
Droo ya Afcon2015 yatangazwa Droo ya Kufuzu kwa kombe la mataifa Afrika mwakani{ Afcon} imefanyika huko cairo Misri huku timu zote za kanda ya Afrika Mashariki zikiratibiwa kucheza katika mechi za mchujo kabla ya kushirikimechi za kufuzu .

NGORONGORO HEROES YATAKATA UWANJA WA TAIFA

Picha
Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania U-20, Ngorongoro Heroes imefuzu kucheza raundi ya pili ya kusaka kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana baada ya kuichapa Kenya kwa penalti 4-3 jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo wa marudiano ulishuhudia Ngorongoro wakilazimishwa sare 0-0 na Kenya kama ilivyokuwa katika mchezo wa kwanza ndipo changamoto ya mikwaju ya penalti ikatumika.

SUAREZ ALAMBA TUZO YA UCHEZAJI BORA EPL

Picha
Mchezaji bora mwaka huu Mshambulizi wa Liiverpool Luis Suarez, ametajwa kuwa mchezaji mwenye tajriba na maarifa ya hali ya juu mwaka huu. Suarez mwenye umri wa miaka 27 alisafiri kuelekea katika sherehe hizo baada ya wao kushindwa na timu ya Chelsea.

JOGOO ALIWA NA MOURINHO ANFIELD

Picha
Demba Ba mfungaji wa bao la kwanza la Chelsea dhidi ya Liverpool Chelsea vijana wa darajani Stanford, jijini London, wamewanyamazisha vinara wa ligi kuu ya England, Liverpool baada ya kuwachakaza mabao 2-0 katika uwanja wao wa Anfield. Liverpool ikiwa imeuanza mchezo huo kwa kasi na kwa dhamira ya kupata ushindi ilishuhudia jahazi lake likitota katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza.

JUDE OKOYE AMTETEA LOLA OMOTOYA

Picha
Kaka wa  P-squre Peter na Paul Okoye ameongea na vyombo vya habari juu ya ugomvi uliotokea wiki iliyopita na kusema kuwa watu wengi wamekuwa wakimnyooshea kidole mke wa Peter ambaye ni pacha wa Paul na kudai kuwa alikuwa chanzo cha ugomvi wa mapacha hao. Jude Okoye alidai kuwa Lola hakuwa na makosa na wala si chanzo cha ugomvi huo hivyo basi wananchi wa Nigeria waache kumnyooshea vidole na kumlaumu. Toka ugomvi utokee wa mapacha hao Lola amekuwa akitumia mesage za lawama na matusi kutoka kwa mashabiki wa Psqure wakidai kuwa mke wa Peter ndiyo chanzo cha ugomvi wa mapacha hao.

SWEBE AWALAANI WAUZA SURA KWENYE SANAA

Picha
Na Regina Mkonde Msanii mkongwe wa hapa nchini kutoka kundi la Kaole Kwanza maarufu kama Swebe Santana (Pichani) alisema kuwa kazi nyingi za sanaa zinashindwa kuendelea na kufahamika kimataifa kwa kuendekeza kuuza sura badala ya kufanya sanaa. Swebe aliongeza kuwa wasanii wengi na wadau wengi wa sanaa hapa nchini hawaangalii uwezo na kipaji cha mtu katika sanaa bali wanachoangalia ni umaarufu na sura ya mtu huku wenye vipaji vyao kukosa nafasi.

MAKALA: TFF BORA LIENDE, UTEUZI WA AJABU TIMU YA TAIFA

Picha
Na Prince Hoza MWISHONI mwa wiki iliyopita Tanzania iliadhimisha miaka 50 ya muungano wake uliotokana na mataifa mawili Tanganyika na Zanzibar ambapo waliunda taifa moja ambalo ni Tanzania. Muungano huo umeweza kudumu kwa miaka 50 ambapo waasisi wa mataifa hayo mawili yaliyoungana nikiwazungumzia baba wa Taifa hayati Mwl Nyerere na hayati Abeid Amaan Karume, wote hao kwa sasa wametangulia mbele ya haki lakini tutawakumbuka sana kwa kutuletea muungano huo. Licha ya muungano huo uliotimiza miaka 50 kutizamwa kwa jicho baya na baadhi ya Watanzania wachache ambao wamekuwa wakiujadili mara kwa mara, kuna wengine wakitaka uvunjwe huku pande nyingine zikitaka muungano wa mkataba.

AZAM FC YAVURUGA MAPATO YA SIMBA NA YANGA

Picha
Kuibukia kwa mafanikio kwa timu ya Azam FC na kufanya vibaya kwa miamba ya soka nchini kumeanza kuzipa machungu ya kiuchumi timu za Simba na Yanga, ambazo katika mechi iliyopita baina ya watani hao wa jadi ziliingiza mapato kiduchu ya Sh. milioni 130, ambayo ni madogo zaidi kupatikana katika miaka ya karibuni tangu ulipojengwa uwanja mpya wa Taifa 2007. Katika taarifa ya uongozi wa Simba iliyotolewa mwanzoni mwa wiki kuhusu tathimini yao kwa msimu huu, katibu mkuu wa klabu hiyo ya Msimbazi, Ezekiel Kamwaga alisema walikuwa wakiambulia mgawo wa mapato wa hadi Sh.300,000 katika baadhi ya mechi zao ikiwamo dhidi ya Ashanti United ambayo walilala 1-0.

REKODI TATA ZA MOYES HIZI HAPA, FERGUSON AMTAFUNA KISOGO

Picha
Moyes ameonekana kutofanya vyema na ndio maana akatimuliwa David Moyes amefutwa kazi na Manchester United baada tu ya miezi kumi kama meneja wa klabu hiyo. Rekodi ya Moyes sio kitu ikilinganishwa na miaka 26 ya usukuni wa Alex Ferguson katika klabu hiyo. Anaaga klabu hiyo ikiwa imeshikilia nafasi ya saba. Pia itakosa fursa ya kucheza katika ligi ya mabingwa wa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1995 na pia wako katika hatari ya kukosa kushiriki michuano ya bara ulaya tangu mwaka 1990.

REAL MADRID YAILAZA BAYERN MUNICH 1-0

Picha
Mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos (kulia) anaruka hewani kuugonga mpira katika UEFA Champions League hiyo jana.  Japo ni kwa ushindi finyu wa bao 1 bila - Real Madrid wamejiwekea akiba nzuri kibindoni na ndiyo watakayoendeleza nayo kampeni yake ya kuwania kuipokonywa ubingwa wa Champions league Bayern. Karim Benzema ndie alitingisha wavu wa Bayern mapema katika kipindi cha kwanza. Mashambulio ya Christino Ronaldo yalikuwa yakisisimua lakini hayakuzaa matunda zaidi kwa Real. Juhudi za Bayern za kukomboa bao hilo zilizimwa kabisa - hivyo kuiwezesha Real kuendeleza rekodi yao ya kutoshindwa nyumbani kufikia mechi 18 .

UTAJIRI WA UWOYA WACHUNGUZWA, MWENYEWE AJIBU MAPIGO

Picha
INADAIWA kuwa hali ya hewa imechafuka kwa msanii nyota wa filamu za Bongo Irene Uwoya ambapo ameshindwa kutaja vyanzo vya utajiri wake wa Ghafla. Hivi karibuni Uwoya alikaririwa akisema kuwa hawezi kutaja kazi nyingine anayofanya na utajiri aliokuwa nao kwani wapo baadhi ya watu hawapendi kuona mmoja wao akiendelea. ...Alisema kuwa pamoja na magari anayomiliki ya kifahari hawezi sema ni njia gani amepata utajiri huo, 'Nimefanya Filamu kadhaa ambazo zimenipa hela na cha zaidi ni Jina ambalo limenifanya kupata Dili zingine zinazonipa Pesa;, alisema na kuongeza.

MAMBO UWANJANI YANG'ARA KIMATAIFA, DIAMOND, MOSES OLOYA WATIKISA

Picha
Na Elias John MTANDAO wa Mambo Uwanjani unaomilikiwa na Prince Hoza ambao umefikisha mwaka mmoja tangia kuanzishwa kwake umeweza kung'ara hasa kutokana na idadi kubwa ya wasomaji wake ndani na nje ya Tanzania. Hadi sasa mtandao huo umetazamwa na watu wasiopungua milioni moja huku nchi za Tanzania, Marekani, Uingereza na Uholanzi zikiongoza kwa kuwa na watazamaji wengi zaidi duniani. Nchi ya Kenya inafuatia kwa ukanda wa Afrika mashariki wakati India inaongoza kwa upande wa bara Asia, takwimu hizo zilizotolewa kufuatana na mpangilio wa utazamwaji wa mtandao huo wa habari unaonyesha kuwa nchi za Ulaya na Amerika ndizo zenye watazamaji wengi zaidi.

SAMATA, ULIMWENGU WAITOSA TAIFA STARS

Picha
Wachezaji  wawili wa kimataifa, Mbwana Samata, na Thomas Ulimwengu, wanaoichezea Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hawatakuja nchini kuivaa Burundi katika mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji Taifa Stars itakayopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, imefahamika. Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Lubumbashi, DRC, Samata alisema wana taarifa ya mchezo huo lakini hawajui kama watakuja kucheza mechi hiyo ambayo haiko kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa). Samata alisema timu yao inakabiliwa na mechi ya ligi itakayochezwa Jumapili dhidi ya Klabu ya Don Bosco, na kwamba uongozi wa TP Mazembe haujawaeleza lolote kuhusiana na ruhusa ya kurejea nchini kuivaa Burundi.

REAL MADRID KUWAKOSA BALE NA RONALDO LEO

Picha
WINGA Gareth Bale yuko shakani kuichezaea Real Madrid katika Nusu Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa mafua. Nyota huyo wa Wales hajasafiri na wenzake kwa ajili ya mchezo wa kwanza leo Uwanja wa Sangtiago Bernabeu. Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti pia anatilia shaka uzima wa Cristano Ronaldo. Nyota huyo wa Ureno anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya muda mfupi kabla ya mchezo wa leo. Ikiwa Bale ataukosa mchezo wa leo, litakuwa pigo kwa Ancelotti, ambaye alimwagia sifa nyingi winga huyo katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wa leo.

CHELSEA YAIBANA ATLETICO MADRID KWAO

Picha
CHELSEA imelazimisha sare ya bila kufungana na Atletico Madrid katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Vicente Calderon. Maana yake, Chelsea itahitaji ushindi mwembamba katika mchezo wa marudiano Uwanja wa Stamford Bridge, London dhidi ya timu iliyoitoa Barcelona katika Robo Fainali ili kutinga Fainali.

CHIFU PANDUKA KUVAMIA JIJI LA TANGA

Picha
MNAJIMU na mganga maarufu wa tiba asilia nchini ambaye pia ni mtabiri wa michezo Juma Mwema au Chifu Panduka (Pichani ) anatarajia kutembelea jiji la Tanga kwa ajili ya kuwasaidia watu mbalimbali wenye matatizo. Akiongea na Mtandao huu mapema leo, Panduka amesema anakwenda Tanga kuwapa huduma wateja wake waliokuwa wakimsubiria kwa muda mrefu. 'Tanga nina watu wengi sana ambao walikuwa wakiniomba niende kuwasaidia, kuna jamii inaishi kwa mashaka lakini inashindwa jinsi ya kusaidiwa, lakini waliponigundua wakaniomba nikawasaidie', alisema. Panduka anasifika kwa kutibu magonjwa mbalimbali pia ana uwezo wa kumjua jini aliye mwilini au mashambani, pia ana uwezo wa kutoa mapepo na majini yalishindikana hasa yale yaliyotegwa makaburini ambayo huzuia riziki za watu. Mtaalamu huyo anayepatikana Tabata Relini jirani kabisa na Hai Bar anatarajia kuwasili Tanga Mei mosi na kurejea jijini Dar es Salaam mei 7 ambapo ataendelea na shughuri zake.

MAASKOFU WATAKA SERIKALI TATU

Picha
Maaskofu 32 wa Kanisa Katoliki Tanzania, wametoa waraka maalumu wa Pasaka wakiwataka wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kuheshimu maoni ya Watanzania yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na kuweka pembeni itikadi za kisiasa katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya. Kupitia tamko lao la pamoja walilolitoa jana na kulipa jina la “Ujumbe wa kichungaji wa Pasaka kwa waamini na watu wote wenye mapenzi mema,” maaskofu hao walisema hivi sasa kuna makundi yenye nguvu ambayo yameanza kushinikiza kuingizwa mambo yenye masilahi kwao kwenye Katiba Mpya. “Tunalisihi na kulishauri Bunge Maalumu la Katiba kuheshimu mawazo yaliyowasilishwa na kutumia busara zilizopendekezwa za kujenga muundo wa Muungano utakaokidhi mahitaji ya utangamano, mshikamano, amani, maadili, uhuru na uwajibikaji wa viongozi na raia wa Tanzania,” walisema katika tamko hilo ambalo, Makamu wa Rais wa TEC, Askofu Severine Niwemugizi alithibitisha kuwa umetolewa na kanisa hilo.

MBUYU TWITE AWEKA HADHARANI UCHAWI WA SIMBA

Picha
DUNIANI kuna mambo, kwani beki wa Yanga Mbuyu Twite amesema inawezekana mashabiki jukwaani waliokuwa wakifuatilia mechi yao dhidi ya Simba juzi Jumamosi waliona kila kitu kinaenda sawa kwao,lakini ukweli ni kwamba yeye na wachezaji wenzake walikuwa wanajiona wazito kiasi cha kucheza chini ya kiwango. Mechi hiyo ya mwisho ya msimu wa Ligi Kuu Bara wa 2013/14 iliisha kwa sare ya bao 1-1, iliishuhudia Simba ikitawala sehemu ya kiungo kwa muda fulani kwa wachezaji wake Jonas Mkude na Said Ndemla kucheza wanavyotaka mbele ya Frank Domayo na Hassan Dilunga. Lakini beki wa kulia wa Yanga, Twite alisema: “Tulikuwa hatujielewi uwanjani, ndiyo maana kuna wakati Simba walionekana kutawala sana kiungo maana ni kama tulifungwa mawe hivi, tulikuwa katika wakati mgumu tukiwa vyumbani wakati wa mapumziko baada ya kila mchezaji kulalamika kujiona mzito. “Pumzi zilitubana muda wote hasa tuliokuwa tunakimbia sana uwanjani, nilishangaa sana kwani kabla ya kuja uwanjani hatukujisikia hivyo.”

AZAM FC YAHAMISHIA MAKALI YAKE KLABU BINGWA AFRIKA

Picha
Baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2013/14, benchi la Azam FC limewapa likizo ya wiki saba wachezaji wake ili wapumzike kabla ya kuanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi hiyo 2014/15 na mashindano ya kimataifa. Azam FC imetwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa mara ya kwanza tangu ipande Ligi Kuu 2007 baada ya kumaliza kileleni ikiwa na pointi 62 ilizozipata bila kupoteza hata mechi moja kati ya mechi 26 zote za ligi.

AIBU MABONDIA WA TANZANIA, WOTE WANUSURIKA KUUAWA

Picha
BONDIA Francis Miyeyusho amepigwa na mpinzani wake, Sukkassem Kietyongyuth wa Thailand kwa Knockout (KO) raundi ya kwanza sekunde ya 55 katika pambano la raundi 10 lisilo la ubingwa, uzito wa Feather lililofanyika ukumbi wa PTA, Temeke, Dar es Salaam usiku wa jumamosi. Katika pambano hilo lililohudhuriwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova aliyekuwa mgeni rasmi, Miyeyusho aligoma kupanda ulingoni kwa dakika zaidi ya 20 akishinikiza kwanza alipwe fedha zake. Kamanda Kova ambaye mdogo wake, Mussa Kova ndiye aliyeandaa mapambano hayo kupitia kampuni yake ya Mawenzi Production, aliingilia sakata hilo na bondia huyo akalipwa fedha zake akapanda ulingoni.

LIVERPOOL YANUSA UBINGWA ENGLAND

Picha
Liverpool ndio washindi watarajiwa wa ligi ya Uingereza baada ya Kuishinda Norwich City mabao matatu kwa mbili katika mechi iliyochezwa wikendi. Kwa sasa Timu ya Liverpool iko na pointi tano zaidi, wakiwa wangali wana mechi kadhaa za kucheza ikiwemo ile ya Chelsea. Japo Chelsea wamesalia katika nafasi ya pili walishindwa kujiimarisha hapo jumapili na kusababisha kuwepo kwa mwanya huo mkubwa baada ya kushindwa na timu ya Sunderland kwa mabao mawili dhidi ya lao moja.

LOGARUSIC AWAAHIDI USHINDI SIMBA KESHO

Picha
Kocha wa Simba, Zdavko Logarusic, amewatoa shaka mashabiki wa timu hiyo waliopoteza furaha kwa kuwaambia kuwa kipigo alichoipa Yanga katika pambano la Nani Mtani Jembe atakiendeleza kesho. Simba na Yanga zitashuka uwanjani kesho kukabiliana katika moja ya mapambano ya hitimisho la Ligi Kuu Tanzania Bara litakalopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba, wameambulia patupu msimu huu baada ya Azam FC kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake, huku wapinzani wao, Yanga wakivuna nafasi ya pili.

TAIFA STARS MPYA YATAJWA

Picha
Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza majina ya wachezaji 16 waliochaguliwa katika maboresho ya timu ya Taifa Taifa Stars kwenye hoteli ya Hill View jijini Mbeya. Wachezaji hao ni kipa Benedicto Tinoko Simwanda (Temeke), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala). Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara).

STURRIDGE HUENDA AKAIKOSA NORWICH

Picha
Daniel Sturridge Straika wa Liverpool Daniel Sturridge huenda asisafiri na viongozi hao wa Ligi ya Premia kwenda Norwich City Jumapili kutokana na jeraha la misuli. Fowadi huyo wa Uingereza alilazimika kuondoka uwanjani dakika ya 66 wakati wa ushindi wao wa 3-2 dhidi ya wapinzani wao ligini Manchester City mnamo Jumapili kutokana na kilichoonekana kuwa jeraha la misuli ya paja. "Sturridge amefanyiwa uchunguzi zaidi na matabibu wa klabu Melwood na jeraha ndogo lilionekana baada ya uchunguzi huo,” Liverpool walisema kupitia taarifa kwenye tovuti yao (wwww.liverpoolfc.com) mnamo Jumatano. Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea na Manchester City mwenye umri wa miaka 24 amefunga mabao 20 msimu huu na kuunda ushirika wa kufana na strika wa Uruguay Luis Suarez ambao umefanya Liverpool kukaribia sana kushinda taji lao la kwanza la ligi tangu 1990.

YANGA ITAIFUNGA SIMBA KESHO BILA OKWI, NIYONZIMA

Picha
YANGA SC imeingiza wachezaji 20 kambini eneo la Bahari Beach kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu, Simba SC kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kukamilisha msimu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Kwa mujibu wa taarifa ya kwenye tovuti ya klabu hiyo jana, wachezaji walioingia kambini ni makipa; Deogratius Munishi ‘Dida’ na Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Ibrahim Job, Rajab Zahir, Kevin Yondan na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, wakati viungo ni Frank Domayo, Hassan Dilunga, Salum Telela, Hamisi Thabit na Nizar Khalfan na washambuliaji ni Didier Kavumbagu, Mrisho Ngassa, Jerry Tegete, Hamisi Kiiza, Hussein Javu na Simon Msuva.

MANISPAA ILALA YAIPIGA MARUFUKU YANGA KUJENGA UWANJA JANGWANI

Picha
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa amepigilia msumari wa mwisho kwa kuwataka Yanga kusahau kuhusu ongezeko la eneo la kujenga uwanja wake eneo la Jangwani kwa vile sehemu hiyo ni mkondo wa maji. Akizungumza, Dar es Salaam jana, Silaa alisema: “Tumepata hasara kubwa (Serikali) hii yote imetokana na watu kujimegea maeneo na kujenga kwenye mkondo wa maji, mafuriko yote haya yanayotokea ni kwa vile maji yanakosa pa kwenda na kuishia kwenye maeneo mengine ndiyo maafa yote haya yanatokea.

BUNGE LA KATIBA KUVUNJIKA

Picha
Hatua ya baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba kususia vikao vya Bunge hilo imezua hofu kwamba inaweza kukwamisha mchakato wa kupatikana kwa Katiba mpya hasa katika kufanya uamuzi wa kupitisha ibara za Katiba hiyo. Wajumbe ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), juzi walitoka nje na kususia vikao vya Bunge hilo kwa madai kwamba hawaridhishwi jinsi mambo yanavyokwenda. Kanuni za uendeshaji wa Bunge hilo za 2014, zinasema ili ibara au Rasimu ya Katiba iweze kupitishwa itahitaji kuungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe kwa pande zote za Muungano.

ANELKA KUTOCHEZA BRAZIL

Picha
Nicholas Anelka Klabu cha Brazil Atletico Mineiro kimetangaza wamefutilia mbali mipango ya kumsaini straika wa Ufaransa, Nicolas Anelka. Mkurugenzi wa timu hiyo Eduardo Maluf amesema kuwa Mineiro wameshindwa katika juhudi zao za kuwasiliana na mshambuliaji huyo aliyechezea Arsenal, Real Madrid, Paris Saint Germain na Chelsea na wamekata tama ya kusajili nyota huyo aliye na umri wa 35. “Hakuna wakati tulifanikiwa kuzungumza naye,” vyombo vya habari vya Brazil vilinukuu Maluf akisema. Miniero walidhibitishia AFP kuwa Anelka hatajiunga na gwiji wa Brazil, Ronaldinho, anayesakata kabumbu yake kwenye timu hiyo huku Maluf akiongeza watatuma malalamishi kwa shirkisho la soka duniani, FIFA, kuhusu straika huyo.

SIMBA KIMEELEWEKA TAYARI KUIUA YANGA JUMAMOSI

Picha
Mjumbe wa kuteuliwa wa Kamati ya Utendaji ya Simba na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo,Zacharia Hanspoppe. Mjumbe wa kuteuliwa wa Kamati ya Utendaji ya Simba na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hanspoppe jana amesaidia fedha za mishahara ya wachezaji ambao waligoma kwenda Zanzibar bila ya kulipwa. Mjumbe huyo ametoa zaidi ya Sh. milioni 30 kusaidia malipo hayo kutokana na wachezaji kukataa kwenda Zanzibar bila kulipwa mishahara yao na posho kwa ajili ya kujiandaa na mechi yao ya kukamilisha ratiba dhidi ya Yanga itakayofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa.

YANGA YAIENDEA SIMBA BAGAMOYO

Picha
Klabu  ya Yanga ambayo ilirejea jijini Dar es Salaam jana ikitokea Moshi ilikocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Panone FC wakati ikiwa njiani kutokea Arusha, imeweka kambi yake Kawe Beach na imeelezwa kwamba huenda wakahamia Bagamoyo mkoani Pwani kwa ajili ya mechi yao ya kukamilisha ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu wao Simba. Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema jana kwamba aulizwe kuhusu kambi ya timu hiyo akishafika Dar es Salaam akitokea Moshi, lakini mara baada ya kutua walikwenda moja kwa moja Kawe Beach na habari kutoka ndani zilisema kwamba kambi hiyo inaweza ikahamia Bagamoyo.

MAOMBI YA ARSENE WENGER YAJIBIWA

Picha
Man City 2-2 Sunderland Maombi ya kocha ,wa Arsenal Arsene Wenger ya kuitaka Everton ishindwe ilikuisaidia timu yake kufuzu kwa kombe la mabingwa msimu ujao yalitimia hapo jana ,Crystal Palace ilipoilaza Everton mabao 3-2 na kuiruhusu Arsenal kusalia katika nafasi ya nne ikiwa na alama 67 alama moja zaidi ya Everton.

MAKALA: MABEKI WAMEINYIMA UBINGWA YANGA MSIMU HUU.

Picha
Na Prince Hoza LIGI kuu ya Tanzania bara inamalizika mwishoni mwa wiki hii huku bingwa tayari ameshajulikana, Azam fc watoto kutoka Chamanzi wamtawazwa rasmi kuwa ambingwa wa msimu huu baada ya kuivua ubingwa Yanga waliokuwa wakiutetea. Kufanikiwa kwa Azam kulitokana na juhudi zao wenyewe ambazo ziliwawezesha kutwaa ubingwa wao wa kwanza msimu huu, kila la kheri Azam kwa kutwaa ubingwa.

REAL MADRID WATWAA UBINGWA WA COPA DEL REY

Picha
Bale asherekea bao la ushindi dhidi ya Barcelona Timu ya Real Madrid ndio mabingwa wa mwaka huu wa kombe la Copa del Rey . Madrid waliwacharaza wapinzani wao wa jadi katika ligi ya nyumbani La liga Barcelona mabao 2 kwa 1 katika fainali iliyochezwa jana mbele ya mfalme wa Uhispania .

TIMU YA WANAWAKE YA LIVERPOOL MBIONI KUTWAA UBINGWA UINGEREZA

Picha
SIYO kaka zao tu wanaotesa Uingereza, Timu ya wanawake ya Liverpool inayofahamika kwa jina la Liverpool Ladies hivi karibuni imeanza kujiimarisha kiulinzi ili kutwaa kombe la The FA Women's Super League. Timu hiyo ambayo inakabiliwa na mechi kali zidi ya wageni wao Man city Ladies inayotarajiwa kuchezwa kesho tar 17 ambapo Liverpool Ladies watakuwa wenyeji.

WAISLAMU HAWAPELELEZWA NEW YORK

Picha
Kamishna wa polisi New York William Bratton alikutana na wakereketwa wa mpango huo Idara ya polisi mjini New York Marekani, imefunga kitengo chake maalum cha ujasusi ambacho huwapepeleza waisilamu ili kuchunguza kama kuna tisho lolote la ugaidi. Kitengo hicho kilikuwa kinatumia polisi waliokuwa wanavalia nguo za kiraia kusikiliza kisiri mawasiliano ya simu kati ya waisilamu na hata kuzuru maeneo yanayotembelewa sana na waisilamu.

AMISSI TAMBWE AKANUSHA KUIHAMA SIMBA

Picha
Na Regina Mkonde. Straika wa timu ya wekundu wa msimbazi Simba Amissi Tambwe amekanusha taarifa ambazo zilikuwa zinavumishwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba amefanya mazungumzo na baadhi ya timu hapa nchini ili ahame Simba. Maneno hayo aliyazungumza Amissi Tambwe akiwa katika kiwanja cha mazoezi cha Kinesi wakijiandaa na mechi  ya watani wao wa jadi Yanga ambayo itachezwa jumamosi ijayo. 'Mimi sijawahi kuongea na vyombo vya habari juu ya suala hili na hata uongozi wa timu yoyote ile ila ninacho shangaa kusikia kwenye vyombo vya habari kwamba Tambwe anataka kuhama Simba', Alisema na kuongeza straika huyo.

TAZAMA PICHA 6: MABINGWA WAPYA BARA AZAM WALIPOWASILI JANA

Picha
Mashabiki wakiilaki Azam FC jioni ya jana Uwanja wa Ndege Dar es Salaam MAMIA ya wapenzi na mashabiki wamejitokeza jioni ya jana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam kuipokea timu ya Azam FC ikitokea Mbeya ambako jana iliwafunga wenyeji, Mbeya City mabao 2-1 na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

NYOTA MAN UNITED WAPIGWA FAINI KWA UFUSKA

Picha
+17 Kujirusha kumewaponza: Welbeck kushoto akizungumza na demu waliyekuwa wakicheza naye na kulia ni Cleverley WACHEZAJI Danny Welbeck, Tom Cleverley na Ashley Young wamepigwa faini na kupewa onyo kali baada ya kujirusha usiku kucha wakiwa na demu saa kadhaa tu baada ya Manchester United kutolewa katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

SIMBA KWENDA Z,BAR LEO, YANGA YAAPA KUTOFUNGWA TENA NA SIMBA

Picha
Wakati  timu ya Simba itaenda mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuanza kambi ya kuwakabili Yanga, mahasimu wao hao wa jadi wamesema timu yao kamwe haitafungwa kizembe tena kama ilivyokuwa katika mechi yao iliyopita. Yanga ilifungwa kizembe 3-1 dhidi ya Simba katika mechi ya 'Nani Mtani Jembe' kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Desemba 21, mwaka jana, mechi ya 'ndondo' iliyowafukuzisha kazi makocha Ernie Brandts raia wa Uholanzi na mzawa Felix Minziro.

UBINGWA WA AZAM YAIZIMA REKODI YA SIMBA

Picha
Timu ya Azam ambayo juzi ilitwaa ubingwa wa Tanzania Bara kwa msimu wa 2013/14, imeweka rekodi saba kwenye medani ya soka nchini. Azam iliifunga Mbeya City mabao 2-1 kwenye uwanja wa Sokoine na kuweka rekodi ya kuwa timu pekee iliyoifunga timu hiyo kwenye uwanja wake wa nyumbani. Awali, Mbeya City ilikuwa haijawahi kufungwa kwenye uwanja wake wa nyumbani kabla ya rekodi yake kuvunjwa na Azam.

NCHI YASIMAMA KUMZIKA GURUMO LEO

Picha
Wakati Rais Jakaya Kikwete ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mwanamuziki Muhidin Gurumo 'Mjomba', mwili wa gwiji huyo wa muziki wa dansi nchini unatarajiwa kuagwa rasmi leo kuanzia saa 2 asubuhi kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini kwao Masaki kwa ajili ya maziko yatakayofanyika mchana.

PHLPS KUOGELEA TENA

Picha
Michael Phelps kurejea katika mashindano ya uogeleaji Bingwa wa dunia katika mashindano ya uogeleaji, Michael Phelps anapania kurejea tena katika ulingo wa uogeleaji hivi

DROGBA APOTEZA MATUMAINI YA KUENDELEA NA SOKA USONI

Picha
Didier Drogba Nahodha wa Ivory Coast Didier Drogba ambaye atacheza Kombe la Dunia bado anatafakari kuhusu mustakabali wake katika klabu ya Uturuki ya Galatasaray aliyojiunga nayo Januari 2013 baada ya kipindi kifupi Uchina. Straika huyo wa miaka 35 alitia saini mkataba wa miezi 18 ambao utaisha Juni, kukiwa hakuna makubaliano ya kuongeza mkataba huo kwa sasa. Fowadi huyo wa zamani wa Chelsea alisema Alhamisi kwamba anahitaji muda kuchagua kati ya familia yake ambao kwa sasa inaishi Uingereza na soka Uturuki. “Napenda sana soka ya Uturuki na zaidi klabu yangu ya sasa ya Galatasaray,” Drogba alisema. “Napenda pia familia yangu ambayo inaishi Uingereza, na nafikiri nitalazimika kuchagua kati ya maeneo hayo mawili. “Nitahitaji muda zaidi kutafakari na kuamua nitakalofanya.” Drogba amepuuzilia mbali ripoti kwamba yuko karibu kutia saini mikataba na klabu zinazocheza MLS ya Marekani na Serie A ya Ita...

MVUA YAIROGA AZAM JANA, SASA KUPUMULIA MASHINE

Picha
Mechi iliyotakiwa kupigwa jana katika dimba la Mabatini,  Mlandizi mkoani Pwani baina ya wenyeji wa uwanja huo, Maafande wa Ruvu Shooting dhidi ya Vinara Azam fc, lakini mechi hiyo imeahirishwa na inachezwa leo jioni baada ya mvua kubwa kunyesha na kuharibu mandhari ya uwanja. Licha ya Yanga kushinda jana, Azam fc bado wapo kileleni kwa pointi moja zaidi ya Yanga, lakini wana michezo mitatu mkononi. Kama watashinda mchezo wao wa 24 hapo kesho, basi watakuwa wanahitaji pointi tatu tu katika mechi mbili zitakazobaki ili kujitangazia ubingwa msimu huu. Mechi ya leo itakuwa na ushindani mkubwa kwa Azam fc kutokana na rekodi ya Ruvu Shooting katika dimba la Mabatini ambapo wanaonekana kuwa wagumu na hutoa ushindani mkubwa zaidi.

YANGA YAIKARIBIA AZAM KILELENI

Picha
Yanga iliongeza presha dhidi ya vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bar, Azam FC, wakati walipoibwaga Kagera Sugar kwa magoli 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kubakisha pointi moja kuwashika vinara. Hata hivyo, Azam FC yenye pointi 53 wana nafasi ya kurejesha pengo la pointi kileleni kuwa pointi nne tena kwa ushindi katika mechi moja yao ya mkononi watakayoicheza leo dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini baada ya kuahirishwa jana kutokana na uwanja huo kujaa maji kufuatia mvua kubwa zilizonyesha. Refa Isihaka Shirikisho kutoka Tanga kwa kushirikiana na wasaidizi wake Hassan Xani wa Arusha, Agnes Pantaleo wa Arusha, Simon Mbelwa wa Pwani na Kamisaa Isabela Kapela wa Dar ndiyo walioukagua uwanja wa Mabatini na kufanya maamuzi ya kuahirisha mchezo huo.