MAKALA: MABEKI WAMEINYIMA UBINGWA YANGA MSIMU HUU.

Na Prince Hoza

LIGI kuu ya Tanzania bara inamalizika mwishoni mwa wiki hii huku bingwa tayari ameshajulikana, Azam fc watoto kutoka Chamanzi wamtawazwa rasmi kuwa ambingwa wa msimu huu baada ya kuivua ubingwa Yanga waliokuwa wakiutetea.

Kufanikiwa kwa Azam kulitokana na juhudi zao wenyewe ambazo ziliwawezesha kutwaa ubingwa wao wa kwanza msimu huu, kila la kheri Azam kwa kutwaa ubingwa.


Azam ina kila sababu ya kupongezwa kutokana na kuonyesha soka la kuvutia tangia awali na kupigana kwa nguvu zote uwanjani na ndio silaha yao kuu msimu huu ambapo imefanikiwa kuchukua ubingwa wa bara pasipo kufungwa hata mechi moja.

Mwishoni mwa wiki hii timu zote 14 zinaingia uwanjani kucheza mechi zao za mwisho, kama nilivyoanza hapo awali kuwa bingwa ameshapatikana, kivumbi kitakuwepo kwa timu zinazopigania kubaki ligi kuu.

Hadi sasa timu za Rhino Rangers ya Tabora na JKT Oljoro ya Arusha zimeshashuka daraja huku vita kali ikisalia kwa timu tatu ambazo ni Prisons ya Mbeya, Ashanti United ya Dar es Salaam na Mgambo JKT katika kupigania kubaki.

Yanga tayari imeshachukua nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Azam huku vijana wapya wa Mbeya City wao wameangukia nafasi ya tatu na Simba yenyewe imekamata nafasi ya nne.

Lakini mechi itakayovuta mashabiki wengi wa soka nchini ni ile ya watani wa jadi Simba na Yanga itakayopigwa Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa, mechi hiyo haitakuwa na maana yoyote kwani mshindi hatoweza kutibua ubingwa wa Azam wala kupanda hatua nyingine.

Mechi hiyo itakuwa ya kutambiana tu, Yanga hawatakubali kupoteza kwa mara nyingine baada ya kulala 3-1 katika mechi yao iliyochezwa Desemba 21 kwenye uwanja wa Taifa mechi ya kirafiki iliyofahamika kwa jina la Nani Mtani Jembe.

Tayari Simba imeanza maandalizi ya mchezo huo ambao unaonekana kuwa muhimu zaidi kwao ili kulinda heshima yake, Mashabiki wa Simba wameonekana kupoteza imani na timu yao kutokana na matokeo mabovu iliyokuwa ikiyapata katika ligi kuu msimu huu.

Simba imepania kushinda mchezo huo ili kuwafurahisha mashabiki wake na ikiwezekana kulinda kibarua cha mwalimu wao Mcroatia Zdravko Logarusic ambaye anaonekana kupungua morali yake tofauti alivyokuja awali.

Logarusic ameonekana kutoelewana na wachezaji wake ambapo amekuwa akiwatukana matusi makali, hivyo ushindi kwa upande wa Simba unaweza kulinda ajira ya kocha huyo anayeanza kuandamwa na mashabiki.

Lakini Yanga wao ndio wana hasira zaidi baada ya kupoteza ubingwa ubingwa wao msimu huu, Yanga pia ina machungu ya kutolewa mapema katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika na Al Ahly ya Misri huku ikiwa na matumaini ya kuvuka kigingi hicho.

Mashabiki wa Yanga hawatakubali kuiona timu yao ikifungwa tena na Simba, Yanga iliamua kuwatimua makocha wake Ernie Brandts, Fred Minziro na Razack Ssiwa baada ya kufungwa mabao 3-1 na Simba.

Hivyo si rahisi tena kupokea kipigo toka kwa mahasimu wao hao, Tayari kikosi cha Yanga kimeshaingia kambini kujiandaa na mchezo huo na ikiwezekana katika mchezo huo Yanga inaweza kuvuna kalamu kubwa ya magoli.

Katika tathimini zangu za ligi msimu huu kikosi cha Yanga ndicho kilichostahili ubingwa na si Azam kama inavyoonekana, safu ya ushambuliaji ya Yanga ndio inayoongoza kwa upachikaji wa magoli kuliko timu zote 14 zilizoshiriki ligi hiyo.

Yanga tayari imeshafunga magoli 59 huku mabingwa wapya wa ligi kuu wamefunga magoli 47, ni tofauti kubwa kati ya washambuliaji wa Yanga na Azam, pia Yanga ndio timu iliyoweza kupata ushindi mkubwa wa magoli ilipocheza na wapinzani wake msimu huu.

Kikosi cha Yanga kiliweza kuibuka na ushindi mkubwa wamagoli katika mechi zake za ligi kuu hata michuano ya Afrika, Yanga iliifunga Ashanti United mabao 5-1 katika mechi ya ligi mzunguko wa kwanza ikiwa cvhini ya MholanziErnie Brandts.

Katika mzunguko wa pili Yanga ndio iliongezeka makaliambapo iliweza kupata ushindi wa kihistoria tangia uwanja wa Taifa uzinduliwe mwaka 2006, Yanga iliifunga Ruvu Shooting mabao 7-0, ikaendeleza vipigo kwa timu nyingine kama Prisons 5-1, na JKT Ruvu 5-0.

Hapo ndipo utakaposhangaa iweje Yanga imekosa ubingwa licha ya kutoa vipigo vikubwa kama hivyo? kilichoiua Yanga msimu huu ni mabeki.

Mabeki wa Yanga wameshindwa kuisaidia timu hiyo licha kujitahidi kuzuia wasifu7ngwe magoli mengi, ni kweli Yanga haijafungwa magoli mengi ila imeruhusu magoli ya kizembe tofauti ilivyotegemewa.

Ukichunguza kisayansi ukuta wa Yanga umeruhusu magoli ya kizembe kuanzia mechi ya Simba na Yanga iliyoishia 3-3, Yanga na Azam mzunguko wa kwanza ambapo Yanga ililala 3-2, pia ilifungwana Mgambo JKT 2-1 ambapo uzembe wa makusudi wa mabeki wa Yanga ulisababisha kupoteza mchezo ule.

Pia Yanga iliruhusu goli la kusawazisha la vijana wa Azam ulioishia 1-1, matatizo katika nafasi ya ulinzi ndio yaliigharimu Yanga hadi kuutema ubingwa ubingwa wake na kunyakuliwa na Azam FC.

Ushauri wangu kwa benchi la ufundi la Yanga kudili zaidi na mabeki itakapokutana na Simba, Yanga inasumbuliwa na nafasi ya ulinzi na inaweza kuiathili katika mechi hiyo, Simba ina washambuliaji wazuri na wajanja kama Amissi Tambwe, pia ina viungo mahiri ambao wanaweza kuichachafya difensi ya Yanga
na kufunga.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA