REKODI TATA ZA MOYES HIZI HAPA, FERGUSON AMTAFUNA KISOGO
David Moyes amefutwa kazi na Manchester United baada tu ya miezi kumi kama meneja wa klabu hiyo.
Rekodi ya Moyes sio kitu ikilinganishwa na miaka 26 ya usukuni wa Alex Ferguson katika klabu hiyo.Anaaga klabu hiyo ikiwa imeshikilia nafasi ya saba. Pia itakosa fursa ya kucheza katika ligi ya mabingwa wa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1995 na pia wako katika hatari ya kukosa kushiriki michuano ya bara ulaya tangu mwaka 1990.
Mameneja waliowahi kushikilia wadhifa huo kwa muda mfupi sana ni pamoja na Sir Matt Busby aliyekuwa meneja wa klabu hiyo kati ya mwaka 1945-1969 aliyerejea tu kama swala la dharura mwaka 1970, na meneja mwingine Jimmy Murphy aliyeshikilia nafasi ya Sir Matt baada ya ajali ya ndege ya Munich mwaka 1958.
Moyes ni kocha wa tatu katika historia ya klabu hiyo kuingoza kwa muda mfupi zaidi.
Kadhalika Moyes alikuwa kocha wa Everton kwa miaka kumi kwa kuipa ukakasi na kuirejesha katika nafasi nzuri kwenye ligi kuu.
Moyes alitarajiwa kuendeleza ufanisi wa klabu hiyo lakini hiyo ilikuwa changamoto kubwa sana kwake na ndio sababu kubwa ya yeye kutimuliwa.
Sir Alex Ferguson
Moyes, aliyeteuliwa na Ferguson kumrithi mwaka jana, alifutwa kazi baada ya kuhudumu kwa miezi kumi pekee.
Kuanzia sasa Ferguson atahusika katika uteuzi huo pamoja na wanachama wote wa bodi.
Wakati wa miaka yake 26 kwenye usukani wa meneja wa klabu hiyo, Ferguson aliweza kushinda mataji 38 ikiwemo 13 ya ligi ya mabingwa mwaka 1999 na mwaka 2008.
Chini ya uongozi wa Moyes, United wameshindwa katika mechi sita nyumbani , wamepata kichapo katika michuano ya FA na kuhindwa katika michuano ya kombe la Capital One katika nusu fainali.
Man U wanashikilia nafasi ya saba wakiwa wamesalia na mechi nne katika ligi kuu ya Uingereza.