REAL MADRID KUWAKOSA BALE NA RONALDO LEO
WINGA Gareth Bale yuko shakani kuichezaea Real Madrid katika Nusu Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa mafua.
Nyota huyo wa Wales hajasafiri na wenzake kwa ajili ya mchezo wa kwanza leo Uwanja wa Sangtiago Bernabeu.
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti pia anatilia shaka uzima wa Cristano Ronaldo. Nyota huyo wa Ureno anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya muda mfupi kabla ya mchezo wa leo.
Ikiwa Bale ataukosa mchezo wa leo, litakuwa pigo kwa Ancelotti, ambaye alimwagia sifa nyingi winga huyo katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wa leo.
Bale anang'ara kwa sasa, baada ya kufunga bao la ushindi katika fainali ya Copa del Rey dhidi ya Barcelona wiki iliyopita na kocha wake akasema mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 86 kutoka Tottenham atakuwa mkali zaidi msimu ujao Hispania ambao utakuwa wa pili kwake Real.
"Gareth ni mtoto mkali,"alisema Ancelotti. "Anavutia kwa kujiamini kiasi cha kutosha hususani kutokana na bao alilofunga dhidi ya Barcelona katika fainali,"alisema.