MAOMBI YA ARSENE WENGER YAJIBIWA
Man City 2-2 Sunderland
Maombi ya kocha ,wa Arsenal
Arsene Wenger ya kuitaka Everton ishindwe ilikuisaidia timu yake kufuzu
kwa kombe la mabingwa msimu ujao yalitimia hapo jana ,Crystal Palace
ilipoilaza Everton mabao 3-2 na
kuiruhusu Arsenal kusalia katika nafasi ya nne ikiwa na alama 67 alama moja zaidi ya Everton.Wenger ambaye ameshuhudia timu yake ikidorora kutoka nafasi ya kwanza mwezi januari hadi ya tano mapema juma hili amesema hiyo ndiyo ombi lake kuu ya kuhakikisha Arsenal inamaliza katika nafasi ya nne bora na kufuzu
kwa ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao.
Crystal Palace 3-2 Everton
Bao la kwanza lilipachikwa wavuni na Fernandinho kunako dakika ya 2.
Man City 2-2 Sunderland
Ratiba ya Man City
- Mon 21 April: v West Brom (H)
- Sun 27 April: v Crystal Palace (A)
- Sat 3 May: v Everton (A)
- Wed 7 May: v Aston Villa (H)
- Sun 11 May: v West Ham (H)
Nasri ndiye aliyemuokoa kocha Manuel Pelligrini aibu ya kushindwa alipofunga bao la kusawazisha kunako dakika ya 88 ya mechi hiyo.
Kutokana na matokeo hayo Pelligrini sasa anategemea matokeo ya vinara wa ligi hiyo Liverpool na Chelsea kubaini matumani yake ya kutwaa taji la mwaka huu.
The Reds ndio wanaoongoza jedwali la ligi na alama 77 ikifuatiwa na Chelsea ikiwa na alama 75.
Man city inashikilia nambari ya tatu kwa alama 71.