MBUYU TWITE AWEKA HADHARANI UCHAWI WA SIMBA

DUNIANI kuna mambo, kwani beki wa Yanga Mbuyu Twite amesema inawezekana mashabiki jukwaani waliokuwa wakifuatilia mechi yao dhidi ya Simba juzi Jumamosi waliona kila kitu kinaenda sawa kwao,lakini ukweli ni kwamba yeye na wachezaji wenzake walikuwa wanajiona wazito kiasi cha kucheza chini ya kiwango.

Mechi hiyo ya mwisho ya msimu wa Ligi Kuu Bara wa 2013/14 iliisha kwa sare ya bao 1-1, iliishuhudia Simba ikitawala sehemu ya kiungo kwa muda fulani kwa wachezaji wake Jonas Mkude na Said Ndemla kucheza wanavyotaka mbele ya Frank Domayo na Hassan Dilunga.

Lakini beki wa kulia wa Yanga, Twite alisema: “Tulikuwa hatujielewi uwanjani, ndiyo maana kuna wakati Simba walionekana kutawala sana kiungo maana ni kama tulifungwa mawe hivi, tulikuwa katika wakati mgumu tukiwa vyumbani wakati wa mapumziko baada ya kila mchezaji kulalamika kujiona mzito.

“Pumzi zilitubana muda wote hasa tuliokuwa tunakimbia sana uwanjani, nilishangaa sana kwani kabla ya kuja uwanjani hatukujisikia hivyo.”


Kuna taarifa zilizoeleza kuwa na hewa nzito katika chumba cha kubadilishia nguo cha wachezaji wa Yanga na alipotafutwa Daktari wa Yanga, Juma Sufiani alisema: “Kila mchezaji alikuwa akilalamika kuwa amekuwa mzito ghafla, hawakuwa hivyo kabla ya kufika uwanjani, siwezi kuthibitisha moja kwa moja kama kuna kitu kilipulizwa vyumbani au la. Tupe muda tufanye uchunguzi.”

Chanzo Mwanaspoti

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA