SAMATA, ULIMWENGU WAITOSA TAIFA STARS

Wachezaji  wawili wa kimataifa, Mbwana Samata, na Thomas Ulimwengu, wanaoichezea Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hawatakuja nchini kuivaa Burundi katika mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji Taifa Stars itakayopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, imefahamika.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Lubumbashi, DRC, Samata alisema wana taarifa ya mchezo huo lakini hawajui kama watakuja kucheza mechi hiyo ambayo haiko kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Samata alisema timu yao inakabiliwa na mechi ya ligi itakayochezwa Jumapili dhidi ya Klabu ya Don Bosco, na kwamba uongozi wa TP Mazembe haujawaeleza lolote kuhusiana na ruhusa ya kurejea nchini kuivaa Burundi.


"Hatujui kama tutakuja, ila taarifa ya mechi hiyo tunayo, huku tuna mechi kesho (leo) na nyingine Jumapili dhidi ya Don Bosco," alisema Samata ambaye alitua TP Mazembe akitokea Simba.

Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alipoulizwa na NIPASHE kuhusu kuja kwa wachezaji hao, alisema hawatakuja nchini licha ya kuitwa na benchi la ufundi la timu hiyo.

Wambura alisema wamewaita kutokana na heshima yao lakini wanafahamu ni vigumu kuwapata siku hiyo.

"Tumewatangaza katika kikosi lakini hawatakuja," alisema kwa kifupi Wambura.

Kikosi kamili kilichoitwa kujiandaa na mechi hiyo na tayari kipo kambini ni pamoja na makipa, Aishi Manula na Mwadini Ally na Deogratias Munishi wa Yanga, wakati mabeki ni Abdi Banda (Coastal Union), Aidan Michael (Ruvu Shooting), Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili,  Kevin Yondani (Yanga SC) na Said Mourad (Azam).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Frank Domayo (Yanga), Himid Mao (Azam) na Jonas Mkude (Simba) wakati washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance), Haruna Chanongo (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samatta (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).

Wachezaji walioitwa kutoka katika kikosi cha maboresho ni kipa Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).

Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara).

Chanzo Nipashe

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA