NI KIAMA LEO: REAL MADRID V BAYERN MUNICH


Munich, Ujerumani. Mabingwa watetezi Bayern Munich leo watakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha inaichapa Real Madrid wakiwa kwenye uwanja wa wake wa nyumbani ili kujihakikishia kubaki katika mashindano hayo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Miamba hiyo ya Ujerumani haijapoteza mchezo hata mmoja nyumbani katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.

Madrid inashuka jijini Munich ikiwa na faida ya ushindi wa bao 1-0, shukrani kwa bao la dakika ya 19 la Karim Benzema kwenye mchezo wa
Jumatano iliyopita.

Bayern haijawahi kupoteza dhidi ya Real katika michezo yote iliyopigwa mjini Munich, wakiwa na  historia ya ushindi katika michezo minane na sare moja, ikifikisha idadi ya ushindi katika michezo 11 dhidi ya Madrid na jumla ya michezo yote kwa timu hizo kukutana ni 21.

Real wameendeleza kiwango chao kizuri tangu walipoifunga Barcelona katika fainali ya Kombe la Mfalme na kuichapa  Bayern kabla ya kuitandika Osasuna kwa mabao 4-0 juzi.

Mchezaji Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo alithibitisha kuwa yuko fiti kuivaa Bayern baada ya kuwa nje kutokana na maumivu ya misuli na alifanikiwa kufunga mara mbili na kumfanya afikishe mabao 47 aliyofunga msimu huu.

Kwa upande wa kocha Pep Guardiola, ameiongoza  Bayern vizuri na kukubali kuruhusu bao katika michezo yake tisa ya mwisho tangu walipotwaa ubingwa wa Bundesliga, wakiwa na rekodi ya ubingwa huo wa mapema wakiwa na mechi saba mkononi mwezi uliopita.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA