TIMU YA WANAWAKE YA LIVERPOOL MBIONI KUTWAA UBINGWA UINGEREZA

SIYO kaka zao tu wanaotesa Uingereza, Timu ya wanawake ya Liverpool inayofahamika kwa jina la Liverpool Ladies hivi karibuni imeanza kujiimarisha kiulinzi ili kutwaa kombe la The FA Women's Super League.

Timu hiyo ambayo inakabiliwa na mechi kali zidi ya wageni wao Man city Ladies inayotarajiwa kuchezwa kesho tar 17 ambapo Liverpool Ladies watakuwa wenyeji.


Timu za Liverpool ya upande wa kike na kiume zimekuwa zikitikisa michuano inayoendelea huko Uingereza ambapo mpaka sasa timu ya wanawake ya Liverpool inaongoza kwa alama 36 ambapo imeshacheza mechi 14  ikifuatiwa na timu ya wanawake ya Bristol Academy Ladies ikiwa na alama 31 nao pia mpaka sasa wameshacheza mechi 14.

Timu ya wanawake ya Arsenal imeshika nafasi ya tatu kwa alama 30 huku ikiwa imeshacheza mechi 14  vile vile timu ya wanawake ya Birmingham City ikishika nafasi ya nne kwa alama 18 huku ikiwa imesha cheza mechi 14 .

Kwa upande wa Liverpool sasa mambo safi kwa kuwa timu zote zipo vizuri kwa wanaume na wanawake pia mpaka sasa Primier League inaongozwa na timu ya Liverpool yenye alama 77 mabayo imeshacheza mechi 34 naChelsea ikishika nafasi ya pili kwa alama 75 pia imeshacheza mechi 34.

Man city ikiambulia kuwa nafasi ya tatu kwa alama 70 amabayo mpaka sasa imeshacheza mechi 32 timu ya Everton imeshika nafasi ya nne kwa alama 66 ambayo imeshacheza mechi 33.

Timu ya wanawake ya Liverpool inakabiliwa na mechi ngumu hivi karibu ikisha cheza na Man City alhamis hii itacheza na timu ya wanawake ya Chelsea jumapili tar 20 ambapo Chelsea Ladies watakuwa ni wenyeji.

Timu ya Liverpool Ladies inaongozwa na wachezaji machachari wanaoongoza kwa kufunga magori kama mchezaji Natasha Dowie ambaye msimu uliopita alifunga mabao 13 na kuwa mfungaji bora wa kike pia Natasha Dowie alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa kike wa mwaka 2013.

Mpaka sasa hakuna timu ya wanawake ambayo inaweza ikaipokonya Liverpool nafasi ya kwanza asilimia kubwa wote wameshacheza mechi 14.

Liverpool Ladies imeipita alama 5 Bristol Academy Ladies ambayo inashikilia nafasi ya pili huku ikiiacha kwa alama 6 timu ya Arsenal Ladies ambayo inashikilia nafasi ya 3.

Kulingana na viwango vya wachezaji wa Liverpool hakuna timu ambayo inaweza ikaipiku Liverpool kwa asilimia mia na hata kama ikitokea itakuwa imefanya kazi ya ziada.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA