NYOTA MAN UNITED WAPIGWA FAINI KWA UFUSKA

Kujirusha kumewaponza: Welbeck kushoto akizungumza na demu waliyekuwa wakicheza naye na kulia ni Cleverley

WACHEZAJI Danny Welbeck, Tom Cleverley na Ashley Young wamepigwa faini na kupewa onyo kali baada ya kujirusha usiku kucha wakiwa na demu saa kadhaa tu baada ya Manchester United kutolewa katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Wanasoka hao wa kimataifa wa England walipigwa picha jijini Manchester usiku wa Ijumaa iliyopita hadi asubuhibaada ya kurejea kutoka Munich Alhamisi ambako Jumatano walitolewa na Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa.

Kocha David Moyes aliwaita watatu hao kuzungumza nao jana makao makuu ya United, Carrington kabla ya kuwataka wafanye mazoezi ya ziada tofauti na wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Wachezaji wote watatu wamepigwa faini, ingawa haiko wazi kama wamekatwa mishahara ya wiki mbili au tatu.

Moyes, ambaye atamenyana na klabu yake ya zamani Everton Uwanja wa Goodison Park Jumapili, ana mpango wa kutumia Pauni Milioni 150 kusajili mwishoni mwa msimu ili kukijenga upya kikosi chake.

Habari njema kwa Moyes, ni kupata nafuu kwa mshambuliaji Robin van Persie kutoka maumivu yake ya goti.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi ameweka ciedo kwenye Facebook inayomuonyesha akifanya mazoezi peke yake gym.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA