REAL MADRID WATWAA UBINGWA WA COPA DEL REY

Bale asherekea bao la ushindi dhidi ya Barcelona
Timu ya Real Madrid ndio mabingwa wa mwaka huu wa kombe la Copa del Rey .
Madrid waliwacharaza wapinzani wao wa jadi katika ligi ya nyumbani La liga Barcelona mabao 2 kwa 1 katika fainali iliyochezwa jana mbele ya mfalme wa Uhispania .


Kocha wa Madrid Carlo Ancelotti alikuwa anajikuna kichwa kwani mshambulizi wake nyota Cristiano Ronaldo hakuwa uwanjani kutokana na jeraha la mguu na hivyo ikambidi kumchezesha mshambulizi aliyegharimu kitita kikubwa zaidi msimu huu Gareth Bale .

Na alidhibitisha udedea wake alipofuma bao la ushindi zikiwa zimesalia dakika tano tu mechi hiyo kukamilika na hivyo kuisadia kutwaa taji lake la 19 la Kombe hilo la mfalme la Copa del rey.
Real Madrid ilidhibitisha niya yao mapema kwa bao la dakika ya 11 Angel Di Maria .
Real Madrid yasherekea ushindi dhidi ya Barcelona
Lakini ikasawazishwa na bao la Bartra katikadakika ya 68 ya kipindi cha pili.
Bao la ushindi lilifungwa na Gareth Bale dakika tano tu kabla ya mechi hiyo kukamilika .
Bale alitimuka mbio na kumpiku mlinzi wa Barca Marc Bartra katikati ya kiwanja na akafululiza hadi akampiga chenga kipa machachari Jose Manuel Pinto na kuihakikishia Madrid ushindi.

Real Madrid bado iko mbioni kuwania kombe la ligi ya Uhispania, ambapo inashikilia nafasi ya pili na alama 79 alama tatu nyuma ya wakinzani wao Athletico Madrid.

Barcelona ambayo imekuwa ikishuhudia msururu wa matokeo yasiyo ya kuridhisha katika siku za hivi punde inafunga orodha ya tatu bora ikiwa na alama 78.

Madrid sasa inamuda wa kutoka kujiandaa kwa mechi ya nusu fainali ya kombe la mabingwa barani Ulaya dhidi ya mabingwa watetezi Bayern Munich ya Ujerumani.
Mechi nyingine ya nusu fainali ya kombe la mabingwa barani Ulaya itakuwa kati ya Chelsea ya Uingereza dhidi ya Atletico Madrid.

Nusu fainali hizo zitachezwa juma lijalo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA