AMISSI TAMBWE KUTIMKA RASMI SIMBA LEO
Mshambuliaji Amisi Tambwe wa Simba anatarajia kuondoka nchini leo kurejea kwao Burundi kwa ajili ya mapumziko huku akiweka wazi kwamba akifika nyumbani atapata jibu la kujiunga na Yanga, Azam FC au kutimkia Uarabuni huku akiweka wazi nia yake ya kutaka kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Afrika ama Kombe la Shirikisho.
Akizungumza katika mahojiano maalum jijini Dar es Salaam jana mchana, Tambwe ambaye ni mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2013/14, alisema akiwa nyumbani kwake Burundi, atakuwa na muda mzuri wa kufikiri na kuchagua timu sahihi ya kuichezea msimu ujao.
"Bado mimi nina mali ya Simba lakini klabu inatambua pia kwamba ninahitaji kupata maslahi mazuri zaidi. Nimefuatwa na watu waliodai wametumwa na klabu za Yanga na Azam lakini mpaka sasa sijapata jibu la timu ipi niikubalie ofa yake," alisema.
"Kesho (leo) mimi na Kaze (Gilbert) tunatarajia kusafiri kurejea nyumbani kupumzika. Nikishafika nyumbani nitazungumza kuhusu klabu ipi nitajiunga nayo msimu ujao.
Tofuati na Azam na Yanga, pia nimepata ofa ya timu kutoka Saud Arabia," alisema zaidi nyota huyo aliyeifungia Simba magoli 19 katika mechi 23 msimu huu.
Mwishoni mwa wiki, mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Burundi na Kombe la Kagame mwaka jana, Tambwe aliweka wazi nia yake ya kuondoka Simba, na amesema anatamani kucheza katika Ligi ya Klabu Bingwa Afrika au Kombe la Shirikisho, kauli ambayo inaonyesha kuvutiwa kwake na kujiunga na Azam ama Yanga ambazo zitaiwakilisha nchi katika michuano hiyo msimu ujao.
Klabu yake ya Simba imekosa tena nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kumaliza katika nafasi ya nne ya msimimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Tayari uongozi wa 'Wekundu wa Msimbazi' kupitia kwa mwenyekiti wa kamati ya usajili, Zacharia Hanspope umeshasema hautamzuia mkali huyo wa mabao kuvunja mkataba wake na klabu hiyo uliobakisha mwaka mmoja endapo akipata timu itakayompa maslahi mazuri zaidi.