JUDE OKOYE AMTETEA LOLA OMOTOYA

Kaka wa  P-squre Peter na Paul Okoye ameongea na vyombo vya habari juu ya ugomvi uliotokea wiki iliyopita na kusema kuwa watu wengi wamekuwa wakimnyooshea kidole mke wa Peter ambaye ni pacha wa Paul na kudai kuwa alikuwa chanzo cha ugomvi wa mapacha hao.

Jude Okoye alidai kuwa Lola hakuwa na makosa na wala si chanzo cha ugomvi huo hivyo basi wananchi wa Nigeria waache kumnyooshea vidole na kumlaumu.

Toka ugomvi utokee wa mapacha hao Lola amekuwa akitumia mesage za lawama na matusi kutoka kwa mashabiki wa Psqure wakidai kuwa mke wa Peter ndiyo chanzo cha ugomvi wa mapacha hao.


Licha ya hivyo Lola alikuwa kimya na hakutaka kuongea na vyombo vya habari juu ya swala hili kutokana na coment za matusi alizokuwa akizipata toka kwa baadhi ya mashabiki wa Peter na Paul.

Chochote kilichotokea hakisababishwi na mwanamke yeyote,samahani tena samahani acheni kumpa lawama mke wa kaka yangu sababu hana hatia ugomvi wa mapacha hawa hakuwa mkubwa ila vyombo vya habari vya Nigeria vimekuza ugomvi huu na kuufanya kuwa mkubwa ila wanachotakiwa kujua ni kwamba damu nzito kuliko maji hivyo basi wataelewana tu.Alisema kaka wa Psqure Jude Okoye.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA