STURRIDGE HUENDA AKAIKOSA NORWICH
|
|
Straika wa Liverpool Daniel Sturridge huenda
asisafiri na viongozi hao wa Ligi ya Premia kwenda Norwich City Jumapili
kutokana na jeraha la misuli.
Fowadi huyo wa Uingereza alilazimika kuondoka uwanjani dakika ya 66 wakati wa ushindi wao wa 3-2 dhidi ya wapinzani wao ligini Manchester City mnamo Jumapili kutokana na kilichoonekana kuwa jeraha la misuli ya paja.
"Sturridge amefanyiwa uchunguzi zaidi na matabibu wa klabu Melwood na jeraha ndogo lilionekana baada ya uchunguzi huo,” Liverpool walisema kupitia taarifa kwenye tovuti yao (wwww.liverpoolfc.com) mnamo Jumatano.
Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea na Manchester City mwenye umri wa miaka 24 amefunga mabao 20 msimu huu na kuunda ushirika wa kufana na strika wa Uruguay Luis Suarez ambao umefanya Liverpool kukaribia sana kushinda taji lao la kwanza la ligi tangu 1990.
Liverpool wanaongoza wakiwa na alama 77 kutoka mechi 34, mbili mbele ya Chelsea, huku City wakiwa na 71 baada ya sare ya 2-2 na Sunderland Jumatano lakini wakiwa na mechi moja hawajacheza.
Baada ya kuzuru Norwich wanaokabiliwa na hatari ya kushushwa ngazi,
Liverpool watakuwa wenyeji wa wapinzani wao katika kuwania taji Chelsea, kisha wakutane na Crystal Palace ugenini kabla ya kumaliza kampeni yao msimu huu kwa kukabiliana na Newcastle United nyumbani.