BYE BYE YA HAMOSNOTA YAZIDI KUBAMBA

Na Regina Mkonde

WIMBO mpya wa mwanamuziki chipukizi wa miondoko ya kizazi kipya yaani bongofleva Hashim Momba ukipenda Hamosnota (Pichani) uitwao Bye bye umeanza kukonga nyoyo na kuanza kujizolea mashabiki ambao wamek,uwa wakimsapoti na kuzidi kubamba na wimbo huo.

Msanii huyo aliyejiunga katika tasnia hiyo hivi karibuni amesema huo ni wimbo wake wa kwanza lakini tayari ameshaandaa nyimbo nyingine ila ataziachia muda si mrefu mara ya hii ya Bye bye kufanya vizuri, akizungumza na Mambo Uwanjani Blogspot, Hamosnota ambaye pia huvuma kwa jina la Fujo amedai wimbo huo umemsukuma kuingia kwenye muziki kwa nguvu zote.

'Nimeamua kufanya muziki kutokana na kuwepo ndani ya damu yangu, muziki mimi nimerithi kutoka kwa mababu zangu, zamani babu yangu alikuwa akipiga marimba hivyo mimi nikapata aidia na kuamua kuendeleza kipaji kilichokuwepo ndani ya ukoo wetu', alisema na kuongeza.


Tayari wimbo huo unafanya vizuri mtaani ambapo watu kadhaa wamekutwa wakiucheza katika nyumba za starehe pamoja na waendesha pikipiki maarufu bodaboda na bajaji, aidha msanii huyo amedai anataraji kuachia video ya wimbo huo hivi karibuni na anachosubiria kwa sasa na wadhamini wake tu ambao wamemuahidi kumsaidia katika utengenezaji video hiyo.

Msanii huyo anaonekana kuupenda muziki zaidi kwani mwandishi wa habari hizi alimshuhudia akiimba baadhi ya mistari iliyopo ndani ya wimbo huo unaomzungumzia maisha yake binafsi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA