UTAJIRI WA UWOYA WACHUNGUZWA, MWENYEWE AJIBU MAPIGO

INADAIWA kuwa hali ya hewa imechafuka kwa msanii nyota wa filamu za Bongo Irene Uwoya ambapo ameshindwa kutaja vyanzo vya utajiri wake wa Ghafla.

Hivi karibuni Uwoya alikaririwa akisema kuwa hawezi kutaja kazi nyingine anayofanya na utajiri aliokuwa nao kwani wapo baadhi ya watu hawapendi kuona mmoja wao akiendelea.

...Alisema kuwa pamoja na magari anayomiliki ya kifahari hawezi sema ni njia gani amepata utajiri huo, 'Nimefanya Filamu kadhaa ambazo zimenipa hela na cha zaidi ni Jina ambalo limenifanya kupata Dili zingine zinazonipa Pesa;, alisema na kuongeza.


'Jina langu ni Kubwa so lazima liendane na Mali ninazopata..aliendelea kusema uwoya, utajiri wa msanii huyo umeanza kutiliwa mashaka ambapo baadhi ya watu wakitaka uhalali juu ya kumiliki maisha ya kifahari.

Imekuwa ngumu kwa msanii wa filamu wa Kitanzania kuwa na utajiri mkubwa na wa mashaka wakati tasnia hiyo ya filamu ikilalama kukosa haki miliki na kufanya wasanii kunyonywa.

Lakini Uwoya anazidi kutisha kwa mali na fedha jambo ambalo limeacha kizaazaa huku hofu ikitanda juu yake, kuna wengine wanahisi kuwa msanii huyo anafanya biashara haramu

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA