MVUA YAIROGA AZAM JANA, SASA KUPUMULIA MASHINE

Mechi iliyotakiwa kupigwa jana katika dimba la Mabatini,  Mlandizi mkoani Pwani baina ya wenyeji wa uwanja huo, Maafande wa Ruvu Shooting dhidi ya Vinara Azam fc, lakini mechi hiyo imeahirishwa na inachezwa leo jioni baada ya mvua kubwa kunyesha na kuharibu mandhari ya uwanja.

Licha ya Yanga kushinda jana, Azam fc bado wapo kileleni kwa pointi moja zaidi ya Yanga, lakini wana michezo mitatu mkononi.

Kama watashinda mchezo wao wa 24 hapo kesho, basi watakuwa wanahitaji pointi tatu tu katika mechi mbili zitakazobaki ili kujitangazia ubingwa msimu huu.

Mechi ya leo itakuwa na ushindani mkubwa kwa Azam fc kutokana na rekodi ya Ruvu Shooting katika dimba la Mabatini ambapo wanaonekana kuwa wagumu na hutoa ushindani mkubwa zaidi.


Baada ya mechi hiyo, Azam fc mwishoni mwa wiki watasafiri kwenda Mbeya kuwafuata wagonga nyundo wa Mbeya, Mbeya City katika dimba la Sokoine jijini humo.

Hii itakuwa mechi ngumu zaidi kwa kocha Joseph Marius Omog wa Azam fc kwa sababu Mbeya City wapo katika ushindani wa nafasi ya pili msimu huu.

Pia hawana rekodi ya kufungwa katika dimba lao tangu kuanza kwa msimu huu.

Si Yanga wala Simba aliyetoka na pointi tatu katika uwanja huo mgumu kwa timu vigogo.

Baada ya Mbeya, mechi ya mwisho kwa Azam fc itakuwa aprili 19 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA