SUAREZ ALAMBA TUZO YA UCHEZAJI BORA EPL

Mchezaji bora mwaka huu
Mshambulizi wa Liiverpool Luis Suarez, ametajwa kuwa mchezaji mwenye tajriba na maarifa ya hali ya juu mwaka huu.

Suarez mwenye umri wa miaka 27 alisafiri kuelekea katika sherehe hizo baada ya wao kushindwa na timu ya Chelsea.

Suarez

"‘Ligi ya Primia ina wachezaji wengi ambao ni wazuri zaidi na ni jambo la heshima sana wachezaji hawa wakiona mchango wako uwanjani’"
Akizungumuza katika sherehe hiyo Suarez alisema kuwa.
Suarez kufikia sasa amefunga mabao 30 na ndiye anayeongoza matumaini Liverpool kukatisha ukame wa miaka 24 tangu watwae taji la ligi kuu ya Uingereza.

Suarez atakumbukwa zaidi kwa kisa kilichogonga vichwa vya habari duniani baada ya kumngata mchezaji wa Chelsea Branislav Ivanovic.
Suarez alipigwa marufuku ya mechi Kumi baada ya kupatikana na hatia .

Wengine walioteuliwa ni Eden Hazzard wa Chelsea aliyetajwa kama mchezaji mchanga wa mwaka huu.
Daniel Sturridge na naodha wa Liverpool Steven Gerrard walijiunga na Suarez kutokana ushirikiano wao iliyopelekea Liverpool kutajwa kama klabu bora ya mwaka huu.

Waliokuwemo ni pamoja na Kipa wa Chelsea Peter Czech na mlinzi Gary Cahil.
Hata hivyo msururu huo haingekamilika pasipo kuwataja Yaya Toure na Vincent Kompany wote wa Manchester City.

Luke Shaw na Adam Lallan wa Southampton pia wakitajwa katika orodha hiyo naye Seamus Coleman wa Everton akifunga ukurasa huo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA